MAHAFALI YA 9 YA CHUO CHA KODI KUFANYIKA DESEMBA 17, 2016 - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MAHAFALI YA 9 YA CHUO CHA KODI KUFANYIKA DESEMBA 17, 2016

MAHAFALI YA TISAYA CHUO CHA KODI

Chuo cha Kodi kinapenda kuwatangazia wahitimu kwa mwaka wa masomo 2015/2016 na Umma kwa ujumla kuwa Mahafali ya Tisa (9) yatafanyika Ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jumamosi tarehe 17 Desemba, 2016, kuanzia saa Tatu asubuhi. Katika mahafali hayo wahitimu wa programu zifuatazo watatunukiwa astashahada, stashada na shahada:


1. Cheti Cha Uwakala wa Forodha cha Afrika Mashariki(CFFPC)

2. Stashahada ya Usimamizi Wa Forodha na Kodi (DCTM)

3. Shahada Ya Usimamizi wa Forodha na Kodi (BCTM

4. Astashahada ya Uzamili ya Uongozi wa Forodha ya Africa Mashariki (PGCCA)

5. Stashahada Ya Uzamili Katika Kodi (PGDT)

Wahitimu wote wanaopenda kushiriki wanapaswa kuzingatia yafuatayo:


1. Kuthibitisha kabla ya tarehe 8/12/2016, kwa Makamu Mkuu wa Chuo Mipango Fedha na Utawala kwa maandishi kuwa watashiriki.


2. Kulipia kiasi cha shilingi 50,000 kwa ajili ya joho na kuwasilisha stakabadhi ya malipo kwa Makamu Mkuu wa Chuo kabla ya 8/12/2016. Malipo yote yafanyike kupitia Benki ya CRDB, Akaunti  ITA Fee Collection Account No. 0150303205600.


3. Wahitimu waliolipia watachukua majoho na kuhudhuria mazoezi Ukumbini siku ya Ijumaa tarehe 16/12/2016, saa 3.00 asubuhi.


Wahitimu watakaoshiriki watagharimia usafiri na malazi yao kwa kipindi chote watakapokuwa Dar es Salaam kwa ajili ya mahafali.


Tafadhali mjulishe na mwingine.

Wote mnakaribishwa
Imetolwana:
Mkuuwa Chuo, ChuochaKodi Eneo la Viwanda MIKOCHENI "B",
S. L. P. 9321, Dar es Salaam. 
Simu: +255 22 2925100
Baruapepe:ita@tra.go.tz

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages