Fidel Castro, kiongozi wa zamani wa Cuba aliyeongoza mapinduzi ya Kikomunisti, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 90, kakake ametangaza.
"Amiri jeshi mkuu wa mapinduzi ya Cuba alifariki dunia mwendo wa saa 22:29 usiku huu (03:29 GMT Jumamosi)," Rais Raul Castro ametangaza.
Fidel Castro alitawala Cuba kama taifa la chama kimoja kwa karibu miaka 50 kabla ya kakake Raul kuchukua hatamu 2008.
Wafuasi wake walisema alikuwa ameirejesha Cuba kwa wananchi.
Lakini alituhumiwa pia kwa kuwakandamiza wapinzani.
Chini ya uongozi wa Fidel Castro, Cuba ilikuwa na uhusiano maalum na Afrika.
Katika miaka ya 1970 na 80, maelfu ya madaktari na walimu walikwenda Afrika na idadi sawa ya askari wa Cuba walipelekwa huko kuingilia kati migogoro na wakala wa vita baridi hasa nchini Angola.BBC Swahili
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)