BENKI YA UBA YATOA MSAADA PUGU SEKONDARI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

BENKI YA UBA YATOA MSAADA PUGU SEKONDARI

 wanafunzi wa Pugu sekondari wakishusha kwenye gari vifaa vilivyokabidhiwa nabenki ya UBA kwa ajili ya wanafuzni wenye mahitaji maalum
 Mkurugenzi mkuu wa Benki ya UBA,Piter Makao akiwa meneja operesheni
Omary wakikabidhi mafuta ya ngozi kwa kijana mwenye ulemavu wa ngozi
,Daudi Nyangusi na Meneja ufadhili wa eleimu kutoka TEA , Tito Mganwa.

 Mkurugenzi mkuu wa Benki ya UBA,Piter Makao akiwa meneja operesheni
Omary wakikabidhi vitabu kwa wanafunzi Salum Mohamed na Ramadhani Juma
pamoja na Meneja ufadhili wa eleimu kutoka TEA , Tito Mganwa.

 Wafanyakazi waUnited Bank of Afrika wakiwa katika picha ya pamoja na
wanafunzi wenye ulemavu wa shule ya Sekondari ya wavulana pugu jijini
Dar es Salaam

 afisa masoko wa UBA , Evance Chandarua akimkabidhi begi, Ramadahani Juma

Na  Humphrey Shao

Benki ya United Banko of Africa(UBA), leo imetoa viti Magodoro, Viti,Magongo ya kutembelea na vitabu vya kujisomea kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu ya shule ya sekondari ya wavulana Pugu jijini Dar es Salaam.


Akizungumza wakati wa kutoa vifaa hivyo Meneja wa benki hiyo nchini ,Piter Makao, amesema kuwa wamechagua kutoa vifaa hivyo katika shule hiyo kutokana na mahitaji ya  watoto hao ambao wamekuwa wakisoma katika mazingira magumu. “Vitu hivi ambavyo tumevitoa leo vitasaidia kwa kiasi kikubwa kuwapunguzia watoto hawa  wenye mahitaji maalum kusoma kwa mawazo kwa kujiona kwamba wao ni sehemu hii ya shule kwa kupata mahitaji yao wote kama ilivyo kwa wengine”Amesema Makao Ameto  wito kwa wanafunzi hao kusoma kwa bidii hili  waweze kufanikiwa katika jamii na baada wajivunie kuwa walisoma pugu
wanafaunzi wenye ulemavu wakiwa katika picha ya pamoja ndani ya bwalo la shule hiyo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages