Kampuni ya Agrics imetatua tatizo la upungufu wa vitabu uliokuwa ukiikumba shule ya sekondari Old Shinyanga kwa muda mrefu sasa. Agrics imeisadia shule hiyo ya sekondari yenye kidato cha tano na cha sita ili kuhakikisha wanafunzi mkoani Shinyanga wanapata elimu ilyobora kiurahisi. Kampuni ya Agrics imesapoti juhudi za serikali katika kuhakikisha watoto wanapata elimu iliyobora.
Kampuni ya Agrics inajihusisha na kutoa mkopo wa pembejeo za kilimo kwa wakulima wadogo wadogo hasa vijijini katika mikoa ya Shinyanga, Simiyu na Geita. Lengo kubwa la kampuni ya Agrics ni kuhakikisha wazazi wanapewa ushirikiano mkubwa katika kuhakikisha watoto wao wanakua katika misingi iliyoimara hasa katika suala la afya na elimu. Kupitia lengo hilo Agrics ilitenga fungu kwa ajili ya kutoa ushirikiano kwa wakulima wake kupitia watoto na hivyo kununua vitabu 62 vya kiada kwa ajili ya kidato cha tano na cha sita katika michepuo ya HGK, HKL, HGE na HGL.
Hatua hii ilifuatiwa na ombi la walimu wa shule hiyo kwa kampuni ya Agrics, shule iliomba vitabu hivyo na kuiomba Agrics isaidie serikali katika kuinua shule hiyo. Mkuu wa shule alieleza kuwa baada vikao na wazazi wa wanafunzi hao pamoja na bodi ya shule kukaa na kufikiria ni jinsi gani wanatatua tatizo la ukosefu wa vitabu. Wazazi walishauri kuomba msaada huo kwa kampuni ya Agrics kwani wanatambua lengo na ushirikiano mkubwa wa kampuni hiyo kwa mkulima hasa katika kuhalkikisha mtoto anapata malezi mazuri.
Akiongea kwa niaba ya kampuni hiyo, mkurugenzi mkuu Bwana Jonathan Kifunda aliwapongeza wazazi na walimu kwa jitihada zao za kutafuta namna ya kutatua changamoto badala ya kuisubiri na kuitupia lawama serikali. Pia amewasisitizia wakulima kanda ya ziwa kijikita katika kilimo biashara ambacho kinatija kwa familia nzima hasa watoto kwani kupitia kilimo hicho wazazi wananufaika na chakula cha kutosha pamoja na kuzalisha mazao ya biashara ili kuhakikisha ada za watoto haziwi tena kikwazo cha watoto kutopata elimu.
Wakulima zaidi ya 7,000 wamenufaika na mkopo nafuu wa mbegu za mahindi, alizeti pamoja na mbolea kwa ajili ya msimu huu mpya wakilimo. Agrics huwanufaisha zaidi wakulima kwa kuwapa mafunzo ya kilimo bure kabisa huku mashamba darasa yakitumika kuwa mfano wa vitendo kwa wakulima hao. Lengo la kampuni ya Agrics ni kuhakikisha mkulima wa mkoa wa Simiyu, Shinyanga pamoja na Geita anainuka kiuchumi na kumuendeleza mtoto kwa manufaa ya taifa zima.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)