




Wafanyakazi wakifanya mazoezi ya kuimarisha miili yao chini ya mpango wa Afya Kwanza wa kampuni

Mmoja wa wafanyakazi wa muda mrefu akipokea cheti kutoka kwa Meneja wa Kiwanda,Jemedari Waziri
Meneja wa kiwanda Jemedari Waziri akiongea na wafanyakazi na wageni waalikwa



Wafanyakazi wakizungusha ngao na cheti cha tuzo mitaani


Hivi karibuni kwa mara nyingine kiwanda cha TBL cha Mbeya kilitangazwa kuwa kiwanda bora cha kutengeneza bia barani Afrika na kunukiwa tuzo katika hafla ya SABMiller iliyofanyika nchini Afrika Kusini.
Wafanyakazi wa kiwanda hicho mwishoni mwa wiki waliitumia siku nzima kusheherekea mafanikio hayo makubwa ambayo yaliambatana na kufanya mazoezi chini ya Mpango wa kampuni wa Afya Kwanza,kuandamana mitaani kuonyesha tuzo waliyopata kwa wananchi,kutunuku vyeti kwa wafanyakazi wa muda mrefu pia kulikuwepo na hafla kubwa ya kupongezana iliyohudhuriwa na wafanyakazi na viongozi mbalimbali wa serikali mkoani Mbeya.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)