Katika kutekeleza mkakati wa kampuni wa kutunza mazingira na sera ya wafanyakazi kutumia muda wao kwa ajili ya kazi za kijamii,baadhi ya wafanyakazi wa TBL Group wameungana na viongozi wa serikali na wafanyakazi wa taasisi mbalimbali za kiserikali na za binafsi katika kampeni ya uhamasishaji upandaji miti inaojulikana kama Mti Wangu.
Kampeni hii imezinduliwa leo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh.Samia Suluhu Hassan katika eneo la viwanja vya Gymkhana.
Wafanyakazi wa TBL Group wakiongozwa na Meneja wa Afya na Usalama Renatus Nyanda na Meneja Ufanisi Wa Uzalishaji Charles Nkondola wakishiriki kupanda mti katika viwanja vya Gymkhana eneo la barabara ya Barack Obama ikiwa ni uzinduzi wa kampeni ya ‘Mti Wangu’ iliyozinduliwa na Makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu Hassan
Diwani wa kata ya Kivukoni manispaa ya Ilala Henry Massaba wa pili (kushoto) akimkabdhi mti wa kupanda Meneja Ufanisi wa Uzalishaji Charles Nkondola Charles Nkondola kwa niaba waya wafanyakazi wa TBL Group wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ‘Mti Wangu’ .Kushoto ni Meneja wa Afya na USalama, Renatus Nyanda.
Wafanyakazi wa TBL Group wakishiriki katika zoezi la upandaji miti





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)