Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega akizungumza kwenye mkutano wa baraza la madiwani juu ya kufanya kazi kwa masilahi ya wananchi na sio kupelekwa kama Kondo leo mkoani Pwani.
Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga,Saum Ally Papen ajifafanua jambo kwenye mkutano wa baraza la madiwani leo mkoani Pwani.
.Sehemu ha madiwani.Picha na Emmanuel Massaka.
Na Chalila Kibuda, Mkuranga
Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega amesema kuwa baraza la madiwani wafanye kazi kwa masilahi ya wananchi na sio kupelekwa kama Kondoo.
Ulega ameyasema hayo leo katika baraza la Madiwani wa Mkuranga katika ulidhiaji wa Ekari 250 ambazo zitatimika katika miradi mbalimbali ya Halmashauri hiyo.
Amesema kuwa mchakato wa kupata ardhi hiyo ulianza muda mrefu hivyo ulipofikia ni pazuri kwa watendaji kijipanga.
Aidha amesema wananchi wanataka maendeleo na majukumu hayo ni madiwani nis kuwajibika pamoja na amesema Mkuranga iko nyuma kimaendeleo hivyo kila kiongozi afanye kazi kwa ajili ya Mkuranga.
Nae Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Juma Abeid amesema ukusanyaji wa mapato iko chini hivyo kunahitaji nguvu katika ukusanyaji wa mapato.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)