Magari ya wafanyakazi yafanyiwa zoezi la ukaguzi
Mkaguzi wa magari toka makao makuu Jeshi la Polisi kitengo cha Usalama Barabarani , Muhidini Mohamed akimwelekeza jambo Meneja Uendeshaji , Mauzo na Usambazaji wa TBL Group Martin Wolfaardt,wakati alipokuwa akikagua magari ya wafanyakazi wa TBL Group Masaki jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama.Kulia ni Meneja majengo wa kampuni hiyo Daud Luwilla.
Mkaguzi wa magari toka makao makuu ya jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani , Muhidini Mohamed (wa pili kulia) akifafanua jambo kwa wafanyakazi wa TBL Group wakati alipofika katika ofisi za Masaki jijini Dar es Salaam kwa ajili ya ukaguzi wa magari ya wafanyakazi wa kampuni hiyo . Kutoka kushoto ni meneja uendeshaji , Mauzo na Usambazaji wa TBL Group Martin Wolfaardt , Meneja majengo Daud Luwilla na Afisa Uhusiano na Mawasiliano Amanda walter.
Wafanyakazi wa Tbl Group ,Kutoka kushoto , Meneja majengo wa kampuni hiyo Daud Luwilla na Afisa Uhusiano na Mawasiliano Amanda walter (katikati) wakimuangalia kwa makini Mkaguzi wa magari toka makao makuu ya jeshi la polisi kitengo cha Usalama barabarani ,Muhidini Mohamed wakati alipokuwa akiwaandika stika za magari yao ofisini kwao Masaki jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama.
Mkaguzi wa magari toka makao makuu ya Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani , Muhidini Mohamed (kushoto)akifafanua jambo kwa wafanyakazi wa TBL Group wakati alipokuwa akikagua moja ya magari ya wafanyakazi wa TBL katika ofisi zilizopo Masaki jijini Dar es Salaam ,ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama .Kulia ni meneja uendeshaji , Meneja majengo wa kampuni hiyo Daud Luwilla na Afisa Uhusiano na Mawasiliano Amanda walter.
Meneja majengo wa TBL Daud Luwilla (kulia) na afisa Uhusiano na Mawasiliano wa TBL Group Amanda walter , wakimwangalia kwa makini Mkaguzi wa magari toka makao makuu ya jeshi Polisi kitengo cha usalama barabarani nchini, Muhidini Mohamed wakati alipokuwa akikagua magari ya wafanyakazi kampuni hiyo Masaki jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani.
Meneja Masoko wa TBL Group Fimbo Butalla (anayeendesha gari) akikaguliwa na Mkaguzi wa magari toka makao makuu ya jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani ,Muhidini Mohamed (kushoto) wakati wa zoezi la kukagua magari ya wafanyakazi wa TBL iliyofanyika Masaki jijini Dar es Salaam ,ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama .Kulia ni Afisa Uhusiano na Mawasiliano Amanda walter na Meneja majengo wa kampuni hiyo Daud Luwilla ,





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)