Makampuni yazidi kuwa na mwamko wa kupambana na saratani - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Makampuni yazidi kuwa na mwamko wa kupambana na saratani

Wafanyakazi  kutoka taasisi mbalimbali za serikali na makampuni  binafsi walijitokeza kwa wingi mwishoni mwa wiki kushiriki matembezi ya hisani ya kuchangia matibabu ya saratani katika taasisi ya Saratani ya Ocean Road iliyopo jijini Dar es Salaam.
Miongoni mwa kampuni ambayo wafanyakazi wengi walijitoa muda wao kushiriki katika tukio hilo la hisani ni kampuni ya TBL Group

Baadhi ya washiriki wa matembezi hayo walieleza kuwa wameguswa na changamoto zilizopo katika kukabiliana na ongezeko kubwa la wagonjwa wa Saratani nchini na kuahidi kuwa watazidi kujitoa  kusaidia wahanga wa ugonjwa huu na kufikisha elimu kwenye jamii jinsi ya kuutambua na kuwahi kupata matibabu zinapojitokeza dalili za ugonjwa huu ambao unazidi kusababisha vifo vya wananchi wengi
Washiriki wa matembezi ya kuchangia wahanga wa Saratani ya matiti wakijiandaa kuanza matembezi katika viwanda vya taasisi ya Ocean Road 
 
matembezi yakiendelea
Bendi ya polisi ikiongoza matembezi 
 
 Shamrashamra mbalimbali  za uhamasishaji zilikuwepo
zoezi la kutembea na mazoezi likiendelea

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages