TANESCO YAWAOMBA RADHI WATEJA WA DAR ES SALAAM WANAOPATA UMEME KUTOKA VITUO VYA KUNDUCHI NA MAKUMBUSHO-KINONDONI KASIKAZINI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

TANESCO YAWAOMBA RADHI WATEJA WA DAR ES SALAAM WANAOPATA UMEME KUTOKA VITUO VYA KUNDUCHI NA MAKUMBUSHO-KINONDONI KASIKAZINI

SHIRIKA la Umeme Tanzania ( TANESCO) linapenda kuwataarifu wateja wake wa Mkoa wa Dar es Salaam kuwa leo Jumamosi tarehe 24/09/2016 kumetokea hitilafu katika Kituo kikubwa cha kupooza na kusambaza Umeme cha Ubungo 220kV/ 132kV  na kusababisha kukosekana Umeme kwenye maeneo ya jiji la Dar es Salaam yanayotegemea Vituo vya Kumduchi na Makumbusho.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Uhusiano TANESCO Makao Makuu jijini mapema leo, tayari hatua za kurekebisha hitilafu hiyo zinaendelea kuchukuliwa ambapo mafundi wa TANESCO wanaendelea na kazi ya kurekebisha hitilafu hiyo na umeme utarejea masaa machache yajayo.

Taarifa hiyo inawaomba radhi wananchi kutokana na usumbufu wowote utakaojitokeza.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages