
Kikosi cha mauzo na usambazaji kutoka DARBREW katika picha ya pamoja wakiwa wameshikilia vipeperushi wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Five Star


Dereva kutoka Idara ya Usambazaji akionyesha kipeperushi cha kampeni ya 5 star.
Wengi wafurahia kupata kinywaji katika mazingira ya usafi
Kampeni ya uhamasishaji utumiaji wa bia ya asili ya Chibuku Super inayojulikana kama ‘Five Star’ inayoendelea kufanyika jijini Dar es Salaam na sehemu mbalimbali kinapopatikana kinywaji hiki inazidi kupamba moto na inaendelea kuwezesha wananchi wengi kuelewa ubora wake na kwa jinsi gani kinaleta burudani sambamba na kupunguza gharama za maisha.
Jina la Five Star au Nyota Tano kwa Kiswahili katika kampeni hii ambapo kila nyota inaeleza hali halisia wa bia hii ya asili na ubora wake katika kuitumia.
Nyota ya kwanza inaelezea kuwa Bia ya asili ya Chibuku ni Bia ya asili ya Kiafrikakutokana na jinsi inavyokubalika katika nchi mbalimbali za Afrika kwa kutumiwa na wengi kama kiburudisho baada ya saa za kazi.
Nyota ya pili inaelezea vionjo vyenye kiwango cha juu vya bia ya Chibuku vinavyotokana na mchanganyiko wa malighafi za nafaka zinazotumika kutengenezea kinywaji hiki
Nyota ya tatu inaelezea radha inayoridhisha ya bia ya Chibuku ambayo inapendeza mdomoni na kuleta raha na burudani ya aina yake.
Nyota ya nne inaelezea ubora wa hali ya juu wa bia ya asili ya Chibuku kutokana na kutengenezwa kitaalamu na kuwa na viwango vinavyotakiwa vya ubora usioleta madhara kwa mtumiaji
Nyota ya tano inaelezea kuwa bia ya Chibuku ni kwa ajili yetu sote kutokana na ubora wake inaweza kutumiwa na watu wenye mitindo ya maisha ya aina mbalimbali pia inapatikana kwenye chupa zenye ujazo wa aina mbalimbali,hali ambayo inawezesha mtumiaji kukipata kinywaji hiki kulingana na mfuko wake ulivyo.
Kampeni ya Five Stars inaendelea kufanyika kwenye vilabu na sehemu nyingi inapouzwa bia ya Chibuku Super na inazidi kuwafikia wengi na watumiaji wake kuongezeka , wengi mbali na kuvutiwa na radha nzuri ya bia hii ya asili wanavutiwa kwa jinsi ilivyofungwa na inavyowafikia watumiaji ikiwa katika mazingira ya usafi na wengi wanakiri kuwa Chibuku ni bia ya asili ya kitanzania inayolinda afya za watumiaji wake na kurahisisha maisha





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)