Afisa Mwandamizi wa Trash back atembelea kiwanda cha TBL Group - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Afisa Mwandamizi wa Trash back atembelea kiwanda cha TBL Group

 Afisa Usalama na Afya  wa Tbl Group, Khery Gunzarethy , akimfafanulia jambo  Meneja Biashara na Maendeleo wa kampuni ya Trash back ya Afrika Kusini ,Andrew Murray (kulia) wakati alipotembelea kiwanda cha bia  Ilala jijini Dar es Salaam  kwa ajili ya kujifunza shughuli mbalimbali za uzalishaji wa vinywaji  na utunzaji wa mazingira.
 Meneja Biashara na Maendeleo wa kampuni ya Trash back ya Afrika Kusini ,Andrew Murray (kushoto) pamoja na wafanyakazi wa Tbl Group  kitengo cha Mawasiliano, wakimsikiliza Mpishi Mkuu wa bia , Benjamin Budigila (Kulia )wakati walipotembelea kiwandani hapo Ilala jijini Dar es Salaam
  Meneja Biashara na Maendeleo wa kamapuni ya Trash back ya Afrika Kusini ,Andrew Murray (kulia)  akionyeshwa moja ya kopo la bia liliohifadhiwa kitaalaam  kwenye pipa maalum la utunzaji wa mazingira   na  Mpishi Mkuu wa bia , Benjamin Budigila ( watatu kulia)wakati alipotembelea kiwandani hapo Ilala jijini Dar es Salaam  kwa ajili ya kujifunza shughuli mbalimbali za ujazalishaji wa vinywaji  na utunzaji wa mazingira. Kutoka kushoto ni  Meneja Mawasiliano wa TBL Group. Zena Tenga , Meneja wa shughuli za ustawi  Irene Mutiganzi na Afisa msaidizi wa mawasiliano Abigail Mutaboyerwa.
Mpishi Mkuu wa bia wa TBL Group,Benjamin Budigila (kushoto) akifafanua jambo,  kwa Meneja Biashara na Maendeleo wa kampuni ya Trash back ya Afrika Kusini ,Andrew Murray (kulia) aliyeongozana  na wafanyakazi wa Tbl Group  kitengo cha Mawasiliano,kuhusiana  na maabara ya kiwanda  cha TBL cha Ilala

Meneja wa Biashara na Maendeleo wa kampuni ya Trash back ya nchini Afrika yuko nchini kwa ziara ya kikazi nchini ambapo amefanya ziara ya kutembelea kiwanda cha TBL kilichopo jijini Dar es Salaam ambapo amevutiwa na mkakati wa utunzaji wa mazingira unaofanywa na kampuni hiyo.

Trash back ni kampuni kubwa nchini Afrika ambayo imekuwa ikijihusisha na usafi wa mazingira mijini hususani kuzoa taka na kutoa ushauri wa jinsi ya kusaga  taka na kuzibadilisha kwa matumizi mbadala yenye kuleta manufaa kwa jamii.

TBL Group inao mkakati wa utunzaji wa mazingira ili kupunguza athari za uharibifu wa mazingira kutokana na uzalishaji kwenye viwanda  vyake na tayari inatekeleza mpango wa kusaga takataka zinazozalishwa katika mchakato wa uzalishaji na kuhakikisha zinatumika kwa matumizi mengineyo .

Kampuni pia imekuwa mstari wa mbele kuunga mkono jitihada za serikali za utunzaji wa mazingira ikiwemo kupanda miti na inayo mikakati mbalimbali ya kuendesha miradi ya utunzaji wa mazingira kwa kushirikiana na wadau mbalimbali na katika kupambana na tatizo la taka jijini Dar es Salaam imewaalika wataalamu wa mazingira kutoka Trash Back ili watoe ushauri wa kusaga taka .

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages