Baadhi ya wahitimu wa mafunzo ya ujasiriamali wakitunukiwa vyeti vya ushiriki kutoka Meneja Mauzo wa TBL kanda ya Iringa-Raymond degera
Wafanyabiashara wa rejareja wanaouza bidhaa zinazozalishwa na viwanda tanzu vya TBL Group wa mkoani Iringa wakifuatilia mafunzo ya ujasiriamali yaliyoendeshwa na taasisi ya TAPBDS kwa udhamini wa TBL Group kupitia mpango wake wa Retail Development Programme.
-Ni utekelezaji wa kanuni ya kampuni ya ‘Dunia Yenye Nuru Njema’
Wafanyabiashara wadogo wanaouza bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya kampuni ya TBL Group nchi nzima watanufaika na mafunzo ya ujasiriamali yaliondaliwa na kampuni kupitia mpango wa kuendeleza wajasiriamali wadogo inaoshirikiana nao kibiashara ujulikanao kama Retail Development Programme (RDP).
Mafunzo haya katika awamu hii yatawafikia zaidi ya wafanyabiashara 1,838 kutoka kanda mbalimbali za mauzo za kampuni nchi nzima katika kipindi cha miezi mitatu kuanzia sasa ukiwa ni mwendelezo wa mkakati wa kampuni wa kuwawezesha wabia wake inaoshirikiana nao kibiashara kwa kufikisha bidhaa inazozalisha kwa walaji wa mwisho ili waendeshe biashara zao kwa weredi na kupata mafanikio katika biashara zao.
Mtazamo na moja ya malengo ya kampuni mama ya SABMiller ni ‘Dunia Yenye Nuru Njema’lengo ambalo limelenga kuharakisha ukuaji wa maendeleo ya kijamii kwa kuhakikisha wabia wake wanaouza bidhaa zinazozalishwa na viwanda vyake hususani wafanyabiashara wadogo wanawezeshwa kustawisha biashara zao ikiwemo kuwawezesha kuishi maisha bora na familia kupitia biashara zao na kutoa mchango wa kuendeleza jamii wanazoishi na kufanyia biashara zao”.Alisema.
Mafunzo haya yanaendana na mahitaji ya ujuzi unaopaswa kutolewa kwa wafanyabiashara kulingana na mahitaji yao kutokana na utafiti uliofanywa na kampuni na kubaini maeneo yenye mapungufu na wameandaliwa mafunzo yatakayowawezesha kuwa na uelewa mzuri wa kuendesha biashara zao kwa ufasaha.
Mafunzo yatakayotolewa kwa wafanyabiashara hao ni kuhusiana na mbinu za kufanikisha mauzo ,nidhamu katika matumizi ya fedha , mahesabu sahihi katika biashara , utunzaji sahihi wa vitabu vya hesabu na mbinu za kukabiliana na ujumla ushindani wa kibiashara ya uuzaji vinywaji na ujasiriamali kwa ujumla.
wafanyabiashara wanapata fursa ya kufundishwa masuala ya usafi na mazingira katika maeneo yao ya biashara na kanuni nyinginezo za kibiashara ikiwemo taratibu za uendeshaji biashara kwa kushirikiana na kampuni ya TBL Group na kutambua bidhaa zinazozalishwa na kampuni hiyo na kampuni zake tanzu.
Kampuni pia imekuwa ikibuni kampeni mbalimbali kwa ajili ya kuwawezesha wafanyabiashara wanaouza bidhaa zake lengo kubwa ikiwa ni kuwainua kimaisha na kustawisha biashara zao na kuwajengea uwezo wa kujiamini kibiashara.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)