
Baadhi ya wafanyakazi na familia zao wakifuatilia matukio ya burudani.
Mkurugenzi Raslimali Watu wa TBL Group,Bw.David Magesse amesema mazingira ya amani na utulivu kwa wafanyakazi katika taasisi yoyote ile yanachangia ufanisi wa kazi na hamasa ya kujituma kwa wafanyakazi wake na alishauri kuwa kuna umuhimu wa taasisi mbalimbali kutambua mchango wa familia za wafanyakazi wake.
Bwana Magesse aliyasema hayo wakati akizungumzia tukio la tamasha la familia za wafanyakazi wa kampuni ya hiyo lililofanyika jijini Dar es Salaam ambalo liliwakutanisha wafanyakazi wa kampuni hiyo kanda ya Dar es Salaam pamoja na familia zao ambapo walishinda na familia zao siku nzima na kufurahi kwa pamoja.
“Sisi kama kampuni yenye viwanda siku hii ni muhimu kwetu kwa kuwa inatukutanisha katika mazingira ya nje ya ofisi na inatupa nafasi ya kufahamiana zaidi sisi wenyewe na familia zetu na kujenga umoja zaidi na utaratibu huu ni wa muhimu kwa waajiri wote kwa kuwa familia za wafanyakazi zikiwa na amani na utulivu unawawezesha waajiriwa kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa”.Alisema.
Alisema TBL Group inakahikisha katika kuongeza mori kwa wafanyakazi wake inaandaa programu mbalimbali zinazoendana sambamba na kuhusisha familia za wafanyakazi wake “Tunao mpango wa Afya Kwanza ambao tumekuwa tukiutekeleza kwa kuhusisha pia familia za wafanyakazi ili kuwawezesha kuwa na afya bora”.Alisema.
Bw.Magesse alisema kuwa tamasha la familia la Dar es Salaam ni mwendelezo wa matamasha ya familia ambayo tayari yamefanyika katika mikoa mbalimbali ambako kampuni imewekeza katika mikoa ya Mwanza,Mbeya,Arusha na Kilimanjaro na kuongeza kuwa kampuni inazidi kubuni programu za kuwaweka karibu wafanyakazi wake pia kuziweka karibu familia zao.
Nao baadhi ya wafanyakazi wa Benki wamepongeza kitendo cha kuandaa tamasha hilo na kubainisha kwamba ni sehemu ya kuwawezesha wafanyakazi pamoja na familia zao kufahamiana.Wamesema tukio hilo linawawezesha wafanyakazi kupumzika na familia zao pamoja na wafanyakazi wenzao katika mazingira tulivu na kirafiki na kupumzika akili na kushiriki huku wakipata burudani mbalimbali na michezo .





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)