Treni ya Kampuni ya Reli (TRL) katika Stesheni ya Dar es Salaam kwenda Pugu huduma ambayo imeanza kutolewa leo. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
KHAMISI KUSSA;
TRENI ambayo imeanza kutoa huduma zake kwa safari ya kuanzia Stesheni ya Dar es Salaam hadi pugu, imeanza kutolewa leo katika stesheni hiyo ambayo itakuwa ikitoa huduma kwa mara 3kwa asubuhi na mida ya jioni mara 3 ambayo itaongeza kasi ya uchumi kwa wakazi wa maeneo ya pugu hasa wakiwemo wachuuzi mbalimbali ambao hasa na wachuuzi wa mboga ambao walikua wakitegemea mabasi ya Abiria (Daladala) hayo yalisemwa na chanzo chetu cha habari likicho dokeza , ambapo wengine hufika Ferry kwa majira ya Asubuhi na kuchukua mboga katika Soko la Kimataifa la Samaki Ferry na kuchukua usafiri wa Bajaji na kuwahi usafiri wa treni kwa muda unao uhitaji wengine kufika pugu inakua ni rahisi kutokana na usafiri huo utakua wa haraka tofauti na mabasi, wengine mboga zao huharibika, na chanzo hicho kiliendelea kusema, kwanza anatoa pongezi kwa Rais Magufuli kwa kuteuwa watu makini wanao endana na kasi ya Rais Magufuli
Meneja huyu ambaye jinalake silifaham, naona mwanzo wake anafanya vizuri zaidi na kumuomba aongeze kasi na kuondoa changamoto iliyopo katika usafiri hapa jijini Dar es Salaam kutokana na foleni aweze kuongeza mabehewa na aongeze vituo,chanzo chetu kiliweza kwenda mbali zaidi na kusema, kutokana na aina ya vitu ambavyo TRL wamependekeza hakika wanastaili pongezi na waweze kukumbukwa watu wa wanao ishi maeneo ya kuanzia Kipawa, Jet Lumo, Karakata na Mjimpya chini hivyo chanzo chetu kilitoa ushauri na maombi kwa Uongozi uweze kusaidia kuwepo vituo hivyo katikati ya Vingunguti, kiembembuzi na Airport ili kuwaguasa wakazi hao waishio maeneo hayo, kama wameamua kuweka usafiri huo niwazi wananchi wengi watajitokeza kufanya biashara kwa wakati tofauti ya mabasi ambapo kutwa nzima unakuwa katika usafiri na foleni ya jiji hili, ninaimani kubwa wakitekeleza hayo niwazi wananchi watakuwa na ari ya kuishughulisha kwa lengo la kujipatia kipato na kujikimu kimaisha na ukilinganisha na kauli ya Hapa kazi
Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wakigombania kuingia katika mabehewa baada ya kuanzishwa usafiri huo
Wanafunzi wa Shule Mbalimbali wakiwa ndani ya mabehewa ya Treni ya Kampuni ya
Reli (TRL) katika Stesheni ya Dar es Salaam kwenda Pugu huduma ambayo imeanza kutolewa .
Askari wa kike ambae jina lake halikuweza kupatikana maramoja, akidandia behewa huku Treni ikiwa imeanza mwendo katika kituo ya Buguruni
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)