TANZANIA KUTUMIA DOLA MIL500 KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIA NCHI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

TANZANIA KUTUMIA DOLA MIL500 KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIA NCHI

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira,January Makamba  akifungua warsha ya wadau wa kuhusu ripoti ya taarufa ya mchango wa Tanzania katika juhudi za kimataifa za kukabiliana na mabadiliko ya Tabia ya Nchi uliofanyika jana kwenye ukumbi wa Veta mjini Tanga kulia ni Kaimu Mkurungenzi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia pia mabadiliko ya tabia ya Nchi, Richard Muyungi na kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi
 Kaimu Mkurungenzi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia pia mabadiliko ya tabia ya Nchi, Richard Muyungi akizungumza katika warsha hiyo ya siku mbili inayofanyika kwenye ukumbi wa Veta Mkoani Tanga.
 Baadhi ya washiriki wa warsha ya wadau kuhusu ripoti ya Taarifa ya Mchango wa Tanzania katika Juhudi za Kimataifa za kukabiliana na mabadiliko ya Tabia ya Nchi katika kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa Veta Jijini Tanga wakimsikiliwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira,January Makamba alikuwa akifungua mkutano huo
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira,January Makamba akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa warsha hiyo kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi  kushoto ni
Kaimu Mkurungenzi wa Mazingira kutoka wizarani
 Richard Muyungi
TANZANIA inatarajiwa kutumia takribani dola mil500 hadi ifikapo mwaka
2030 ili kuweza kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi
yanayoendelea katika maeneo mbalimbali hapa nchi.

Kiasi hicho cha bajeti kinatarajiwa kutumika kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ambayo itasaidia kupunguza  juhudi za kupunguza joto zinazosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano
na Mazingira January Makamba wakati wa ufunguzi wa warsha ya wadau
kuhusu ripoti ya taarifa ya mchango wa Tanzania katika juhudi za kimataifa za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Aliitaja baadhi ya miradi ambayo itatekelezwa ili kupunguza gesi
joto hapa nchini kuwa ni dampo la mtoni katika Jiji la Dar Es Salaam,miradi ya nishati jadidifu katika maeneo ya Mbinga,Makete,Njombe Usa River na Ifakara.

“Miradi hiyo yote inajumla ya megawati tano(5MW) za uzalishaji wa hewa ukaa ambapo iwapo hatua za haraka hazitaweza kuchukuliwa athari za
kimazingira zinaweza kuendelea kujitokeza”alisema Waziri Makamba.

Ambapo alisema katika kushiriki  juhudi za kimataifa za kupunguza uzalishaji wa gesi joto tayari serikali ya Tanzania imeshaanza kutoa fursa kwa wadau ya kushughulikia mabadiliko ya tabia nchi .

Makamba alisema kuwa mikakati hiyo kwa sasa imeshaanza kutekelezwa
katika ngazi za mikoa wilaya pamoja na Halimashauri mbalimbali hapa
nchini.

“Juhudi za serikali ni kuhimiza matumizi ya gesi asilia katika uzalishaji wa nishati ya umeme yanaongezeka ili kuweza kupunguza matumizi ya vifaa vinavyozalisha hewa ukaa ili kukabiliana na kasi ya mabadiliko ya tabia nchi”alisisitiza Waziri Makamba.

Kwa upande wake Kaimu Mkurungenzi wa Mazingira kutoka wizarani  Richard Muyungi alisema kuwa sasa wapo kwenye mkakati wa kutoa elimu kwa wadau wa mazingira kwenye kanda mbalimbali nchini.

Alisema ilikuweza kuwa na mipango madhubuti katika utekelezaji
mkakati wa taifa wa mawasilinao wa mabadiliko ya tabia nchi kupitia
wizara za kisekta. 
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages