SHIRIKA la Umeme Tanzania, (TANESCO), linawaomba radhi wateja wake wa Mkoa wa Temeke, kufuatia katizo la umeme usiku wa kuamkia leo Agosti 20, 2016. Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ofisi ya Uhusiano Makao Makuu, sababu za kukatika kwa umeme ni hitilafu iliyotokea kwenye njia ya umeme unaotoka Ilala kwenda Kurasini, natayari mafundi wa TANESCO kutoka mkoa wa Temeke wanaendelea na kazi ya kurekebisha hitilafu hiyo.
Maeneo yaliyoathirika na katizo hilo ni pamoja na Mbagala yote, Kurasini yote, Mtoni yote, na baadhi ya maeneo ya Temeke.
Taarifa hiyo imesema, baada yahitilafu hiyo mara moja mafundi wa TAENESCO waliingia kazini usiku huo huo na hadi kufikia majira ya asubuhi, baadhi ya maeneo kama vile Temeke, na Kurasini umeme ulirejea.
Taarifa hiyo inasema, umeme utarejea katika hali yake ya kawaida kwenye maeneo yote muda mfupi ujao na taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.
Taarifa hiyo imewataka wananchi kutoshika au kukanyaga waya wa umeme uliokatika au kuanguka na pindi uonapo hali hiyo kwenye eneo lako, tafadhali wasiliana na TANESCO kupitia namba zifuatazo, :Kituo cha miito ya simu namba 2194400 au 0768-985100. Shirika linawaomba radhi wananchi kutokana na usumbufu uliojitokeza.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)