Baadhi ya wafanyakazi wa Startimes Tanzania, Mwakilishi wa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Na wasanii Mbalimbali Wakikata Keki kuashiria shangwe ya kutimiza miaka Miwili ya Chaneli ya Startimes Swahili tokea kuanzishwa Kwake. Tamasha hilo lililopewa jina la Serebuka Festival lililofanyika katika Viwanja vya Posta Kijitonyama jana na Kudhaminiwa na Huawei Tanzania.
Msanii kutoka Zanzibar akitoa burudani mbele ya watazamaji waliohudhuria tamasha hilo la Serebuka Festival lililofanyika kwaajili ya kusherehekea miaka miwili ya Chaneli ya Startimes Swahili.
Mshereheshaji wa tamasha hilo Jokate Mwigelo akitoa mawili matatu mbele ya umati wa watu waliohudhuria tamasha hilo
Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar na vitongoji vyake waliohudhuria tamasha hilo huku wengine wakichukua taswira ya matukio yaliyokuwa yakiendelea
Msanii wa Bongo fleva Madee akitoa burudani katika Tamasha hilo hapo jana katika viwanja vya posta kijitonyama
Msanii wa Bongo Fleva Alikiba akikaribishwa jukwaani na baadhi ya wafanyakazi wa startimes Tanzania kwaajili ya kukata keki ikiwa ni ishara ya kusherehekea kutimiza miaka Miwili ya chaneli ya Startimes Swahili kabla ya kuanza kutoa show kwa wahudhuriaji wa tamasha hilo.
Msanii Shaa akitumbuiza mashabiki pamoja na wacheza shoo wake kwenye jukwaa la Serebuka Festival hapo jana
Wacheza shoo wa Alikiba wakiendelea kutoa burudani kwenye jukwaa la Serebuka Festival
Wafanyakazi wa Startimes Tanzania wakipiga selfie na msanii wa Bongo Movie JB wakati wa Tamasha la Serebuka lililofanyika katika Viwanja vya Posta kwaajili ya Kusherehekea Miaka Miwili ya Chaneli ya Startimes Swahili.
Msanii wa bongo fleva Alikiba akitoa burudani katika tamasha hilo.
Mashabiki waliohudhuria tamasha hilo
Juma nature pamoja na Rich One wakikamua kwenye jukwaa la Serebuka Festival jana katika viwanja vya Posta Kijitonyama Jijini Dar Es Salaam
Baadhi ya washindi wa dekoda za Startimes wakipiga picha ya pamoja na Jokate Mwengelo mara baada ya kuibuka kidedea kwenye kujibu maswali yanayohusu Chaneli ya Startimes Swahili hapo jana katika Serebuka Festival.Picha Zote na Josephat Lukaza - Lukaza Blog
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)