Pages

Mkurugenzi wa masuala ya nje ya SABMiller afanya ziara ya kikazi nchini

 
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji Dk,Adhelm Meru akisalimiana na Bw.Monwabisi Fendeso alipowasili ofisini kwake na ujumbe wake kwa ziara ya kikazi
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji Dk,Adhelm Meru katika mazungumzo na Monwabisi Fendeso na ujumbe wake
 Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Private Sector Foundation,Bw.Godfrey Sembeye akibadilishana mawazo na Monwabisi Fendeso kutoka SABMiller Africa walipokutana jijini Dar es Salaam jana
Monwabisi Fendeso na ujumbe wake katika majadiliano na watendaji wa Chama cha Wafanyabiashara

Mkurugenzi wa Masuala ya Nje wa kampuni ya SABMiller kanda ya Afrika,Bw.Monwabisi Fendeso,yuko nchini kwa ziara ya kikazi ambapo atatumia fursa hii kukutana na watendaji wa serikali , taasisi mbalimbali za  na vyama vya wafanyabiashara
 
Bw.Fendeso tayari amekutana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dr.Adelhem Meru, pia amekutana na watendaji wakuu wa chama cha wafanyabiashara wenye viwanda, na Tanzania Private Sector Foundation.
 
Mazungumzo hayo yalihusu mikakati mbalimbali ya kampuni hiyo itakavyoshirikiana na serikali na sekta binafsi kuimarisha sekta ya viwanda na kilimo nchini na sekta ya biashara kwa ujumla.
 

Kampuni ya SABMiller ambayo ni kampuni mama ya kampuni ya TBL Group tayari imeanza kutekeleza programu mbalimbali za kuinua sekta ya viwanda na kilimo nchini ikiwemo programu ya Go Farming ya kuendesha kilimo shirikishi na wakulima ambayo tayari imenufaisha wakulima za zao la Shahiri kanda ya Kaskazini mwa Tanzania na wakulima wa zabibu mkoani Dodoma.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)