Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili kwenye ardhi ya mji wa Mbabane nchini Swaziland tayari kuhudhuria mkutano wa 36 wa SADC wa Wakuu wa nchi na Serikali ambao utafanyika tarehe 29 Agosti mjini hapo.
Sehemu ya Mabinti wa Swaziland wakiimba na kucheza wakati wa mapokezi ya Makamu wa Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokelewa na ngoma mbali mbali mjini Mbabane nchini Swaziland.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kushoto) akizungumza na Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Phiwayinkhosi Mabuza wa Swaziland ambaye pia ni Kaimu Waziri wa Fedha mara baada ya kuwasili kwenye kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Mfalme Mswati III.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewasili mjini Mbabane - Swaziland leo kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa 36 wa Wakuu wa nchi na serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika- SADC.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan atamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano huo ambao utafanyika tarehe 29 Agosti 2016 ambapo Tanzania inatarajiwa kukabidhiwa nafasi ya Uenyekiti wa Jumuiya hiyo.
Mkutano huo wa 36 wa SADC ni maalum kwa wakuu wa nchi na serikali wanaounda Kamati ya siasa,ulinzi na usalama ambao watajadili kwa kina hali ya siasa na usalama, demokrasia na maombi ya Burundi na Comoro kwa ajili ya kujiunga na SADC.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan katika msafara wake amefuatana na Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Kikanda na Kimataifa Augustine Mahiga, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage na Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Amina Salum Ali.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)