MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA UJUMBE WA TAASISI YA HANS SEIDEL JIJINI DAR ES SALAAM - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA UJUMBE WA TAASISI YA HANS SEIDEL JIJINI DAR ES SALAAM


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akizungumza na Mwenyekiti wa Taasisi ya HANNS SEIDEL kutoka nchini 


Ujerumani Profesa Ursula Mannle (kushoto)ambaye ameongoza ujumbe wa watu wanne akiwemo Waziri wa Nchi, Kazi, Masuala ya Kijamii wa Bavaria    Mhe. Emilia Muller walipometembelea Makamu wa Rais Ikulu jijini Dar es 


Salaam.


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akizungumza na Mwenyekiti wa Shirikaka la HANNS SEIDEL kutoka nchini 


Ujerumani Profesa Ursula Mannle (kushoto) pamoja na Waziri wa Nchi, 

Kazi, Masuala ya Kijamii wa Bavaria   Mhe. Emilia Muller 
walipometembelea Makamu wa Rais Ikulu 
jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  (katikati)  
Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na ujumbe kutoka Taasisi ya HANNS  
SEIDEL la Ujerumani,Wengine pichani ni Waziri wa Nchi, Kazi, Masuala ya 
Kijamii wa Bavaria   Mhe. Emilia Muller ( kulia)  Mwenyekiti wa Taasisi ya HANNS SEIDEL kutoka nchini Ujerumani Profesa Ursula Mannle (kushoto), Mwakilishi Mkazi wa Taasisi HANNS SEIDEL Bi. Julia Berger( wa pili kushoto),Meneja wa Mradi Kadele Mabumba (wa pili kulia), Ikulu jijini Dar es Salaam



Makamu 
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan ameitaka Taasisi 
ya Hans Seidel Foundation isaidie kupeleka Elimu ya Uraia bungeni ili wabunge 
wajue wajibu wao ndani na nje ya Bunge.



Mhe. 
Samia ametoa kauli hiyo leo baada ya kukutana na ujumbe wa Taasisi ya Hans 
Seidel Foundation uliomtembelea ofisi kwake Ikulu, Jijini Dar es salaam kutaka 
kujua kama ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuna sheria na 
kanuni za kuendesha vikao vya Bunge. 


Makamu 
wa Rais aliueleza ujumbe huo ulioongozwa na Mwenyekiti wa Hans Seidel 
Foundation Prof. Ursula Mannle kuwa sheria na kanuni zipo za kuendesha vikao vya 
Bunge lakini baadhi ya wabunge hawazifuati kama inavyotakiwa.




Alisema 
kwa mtazamo wake elimu ya uraia itasaidia katika kuwafanya wabunge hao wajenge 
nidhamu katika michango na ushiriki wao kwa ujumla ndani na nje ya Bunge.



Akizungumzia 
kuhusu kuanzishwa kwa dawati la jinsia katika vituo vya polisi Mheshimiwa Samia 
alisema ni hatua nzuri kwani wanawake kwa sasa wako huru kueleza wanapofanyiwa n
ukatili wa kijinsia tofauti na ilivyokuwa hapo awali. 



"Kwa 
sasa wanawake wanakutana na wanawake wenzao wako huru kuzungumza wanaporipoti 
matukio ya kupigwa na haki inatendeka bila ya hata kutoa rushwa. Kuna mabadiliko 
ndani ya Jeshi la Polisi kwa upande huo," alisema Mhe. Samia.



Alisema 
kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano ni kuhakikisha watu wote 
wanaoenda kinyume na taratibu wanachukuliwa hatua za kisheria na kusema kwenye 
utumishi wa umma mambo yamebadilika kiasi kwamba makusanyo ya kodi yameongezeka Serikalini.



Taasisi 
ya Hans Seidel Foundation yenye makao yake makuu Munich, nchini Ujerumani 
ambayo inajishughulisha na masuala ya demokrasia, amani na maendeleo huku 
ikitoa kipaumbele kwenye elimu ya uraia inaendesha shughuli zake katika nchi 
zaidi ya 60 duniani.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages