Wanawake watatu kutoka kampuni ya TBL Group wamechaguliwa kujiunga na mpango wa mwanamke wa wakati ujao ambao imeanzishwa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) kwa kushirikiana na Shirikisho la Vyama vya Waajiri nchini Norway ambao umeenga kuboresha ufanisi wa wafanyakazi wa kike mahali pa kazi hapa nchini.
Mpango huu ambao umezinduliwa jijini Dar es Salaam unawashirikisha wanawake wapatao 33 kutoka makampuni mbalimbali nchini ambao watapatiwa mafunzo mbalimbali ya uongozi.
Akiongea kwa niaba ya wenzake Meneja wa kuendeleza vipaji wa TBL Group Lilian Makau Galinoma ambaye amechaguliwa kushiriki katika mpango huu alisema wanashukuru kampuni yao kwa kuona umuhimu wa kuendeleza wafanyakazi wake.
“Tunaishukuru kampuni yetu kwa kutufadhili ili tuweze kupata mafunzo ya uongozi na tuna imani yatatupa upeo zaidi wa kuboresha utendaji wa kazi zetu za kila siku ikiwemo kuendeleza vipaji vya wafanyakazi wenzetu wa kike “.Alisema.
Meneja wa kuendeleza Vipaji wa TBL Group Lilian Makau Galinoma akitoa mada wakati wa uzinduzi wa mpango wa Mwanamke wa wakati ujao Tanzania ( Female Future Tanzania) ulioanzishwa na na Chama Cha waajiri Tanzania( ATE) .Uzinduzi ulifanyika katika iliyofanyika hoteli ya Sea Cliff jijini Dar es Salaam

Mkurugenzi Mkuu wa Chama cha Waajiri Tanzania ( ATE) Dk.Aggrey Mlimuka (kulia) akimpongeza Meneja wa kuendeleza Vipaji wa TBL Group Lilian Makau Galinoma mara baada ya kumaliza kutoa mada wakati wa uzinduzi wa Progamu ya Mwanamke wa wakati ujao Tanzania ( Female Future Tanzania) iliyoandaliwa na Chama cha waajili Tanzania( ATE) katika hoteli ya Sea Cliff jijini Dar es Salaam

Watendaji waandamizi wa taasisi mbalimbali wakiwa katika picha ya washiriki wa mpango wa Mwanamke wa wakati ujao Tanzania ( Female Future Tanzania) wakati wa uzinduzi wake katika hoteli ya Sea Cliff jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mkuu wa Chama cha Waajiri Tanzania ( ATE) Dk.Aggrey Mlimuka (wa pili kulia ) akibadilishana mawazo na Meneja Vipaji wa TBL Group Lilian Makau Galinoma (wa pili kushoto) wakati wa uzinduzi wa mpango wa Mwanamke wa Wakati Ujao Tanzania ( Female Future Tanzania) utakaoendeshwa na Chama cha waajiri Tanzania( ATE) .Kushoto ni Meneja bidhaa wa Kiwanda cha Konyagi (DTL)Warda Kimaro na Meneja Mkuu mpishi wa pombe wa Chibuku.(DARBREW) Neema Arora. Uzinduzi umefanyikakatika hoteli ya Sea Cliff jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mkuu wa Chama cha Waajiri Tanzania ( ATE) Dk.Aggrey Mlimuka (wapili kulia ) akisalimiana na Meneja Vipaji wa TBL Group Lilian Makau Galinoma (wapili kushoto) wakati wa Warsha ya Mwanamke wa Wakati Ujao Tanzania ( Female Future Tanzania) ulioandaliwa na Chama cha waajiri Tanzania( ATE) katika haoteli ya Sea Cliff jijini Dar es Salaam, leo.Kushoto ni Meneja bidhaa wa Kiwa nda cha Konyagi (DTL) na Meneja Mkuu mpisha wa pombe wa Chibuku.(DARBREW) Neema Arora.
Baadhi ya washirki wa Warsha ya Mwanamke wa Wakati Ujao Tanzania ( FEMALE FUTURE TANZANIA) wakimsikiliza mada mbalimbali zilizotolewa wakati wa uzinduzi wake katika haoteli ya Sea Cliff jijini Dar es Salaam





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)