Pages

Waliokuwa wanafunzi wa Bwawani Sekondari waikumbuka shule yao kwa kuitembelea

 Baadhi ya wanafunzi tuliosoma Shule ya Sekondari Bwawani tukiwa katika picha ya pamoja wakati wa kuelekea kuitembelea shule yetu hiyo..
 Mwalimu Leornad Chintowa akiwakaribisha baadhi ya wanafunzi waliopata kusoma katika shule ya Sekondari ya Bwawani inayomilikiwa na jeshi la Magereza nchini mara baada ya kuwasili kwa waliokuwa wanafunzi wa shule hiyo mapema leo.
 Baadhi ya waliokuwa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Bwawani iliyopo mkoa wa Pwani wakipata maelekezo kutoka Kwa viongozi wa wanafunzi kuhusiana na Maabara mpya iliyojengwa shule hapo kipindi ambacho waliokuwa wanafunzi katika shule hiyo hawakuiacha.
 Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Bwawani wakipiga picha na aliyewahi kuwa mwanafunzi wa shule hiyo na kuhitimu mwaka 2004, Christopher Mwansasu mara baada ya waliokuwa wanafunzi wa shule hiyo kutembelea shule yao kwaajili ya kuwatia moyo na amasa ya kusoma vijana wanaoendelea na masomo shule hapo
 Baadhi ya wanafunzi waliowahi kusoma Shule ya Bwawani na kuishi katika Bweni la Nguvu Kazi wakiwa mbele ya bweni walilowahi kuishi miaka hiyo wakiwa shuleni hapo. Kutoka kulia ni Amosi Kilindo ambaye alihitimu kidato cha nne shuleni hao mwaka 2004 na anayefuata ni Peter Mloka ambaye alihitimu kidato cha Nne mwaka 2005.
Aliyewahi kuwa mchezaji wa netball wa timu ya shule ya Bwawani kuanzia mwaka 2003 hadi mwaka 2006, Maria Plantana akimkabidhi mchazaji wa netball wa timu ya shule ya bwawani Kwa sasa mpira wa Netball ikiwa kama zawadi ya kuwatembelea wanafunzi hao shuleni hapo.
 Maelekezo yakiendelea kwa waliokuwa wanafunzi wa shule ya Bwawani iliyopo Mkoa wa Pwani.
 Aliyekuwa Mwanafunzi wa Shule ya Bwawani, Salome Mathew akipanda Mti kama ishara ya kumbukumbu shule hapo mara baada ya kuwasili shuleni hapo kwaajili ya kuwatia moyo wanafunzi wanaoendelea na masomo
 Kaka Mkuu msaidizi (Mwenye sare) akibadilishana mawazo na waliokuwa wanafunzi katika shule hiyo wakati walipotembelea shule hiyo kwaajili ya kuwatia moyo na amasa wanafunzi wanaoendelea na Masomo katika shule hiyo ya Bwawani inayomilikiwa na Jeshi la Magereza nchini Tanzania wanaoshuhudia Pembeni ni walimu wa shule hiyo 
 Baadhi ya wanafunzi wanaoendelea na masomo shule hapo wakiwa katika Picha ya Pamoja na walimu na baadhi ya wanafunzi waliowahi kusoma katika Shule hiyo ya Bwawani miaka kadhaa iliyopita.
Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha kwanza mpaka cha sita wakiwa katika bwalo la shule kwaajili ya kuwasikiliza waliokuwa wanafunzi wa shule hiyo miaka kadhaa iliyopita ambao waliwatembelea na kuongea nao machache ikiwemo kuwapa moyo na kuwafanya waone umuhimu wa shule pindi wanapokuwa shuleni.
 Baadhi ya wanafunzi waliowahi kusoma katika shule ya Bwawani iliyopo Mkoa wa Pwani wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutembea sehemu mbalimbali za shule hiyo kujionea tofauti 
 Mmoja wa wanafunzi aliyehitimu mwaka 2006, Frank Mushi akipanda Mti mara baada ya kuwasilini shule hapo wakati wa ziara iliyofanya na wanafunzi waliohitimu katika shule ya bwawani huku baadhi ya wanafunzi hao waliowahi kusoma hapo wakitoa zawadi ya mipira kama vile mpira wa miguu, wavu na mpira wa pete, huku wakitoa Miche 30 ya miti ambayo imepandwa shule hapo kama ishara ya kumbukumbu kwa wanafunzi hao
Baadhi ya wanafunzi waliosoma na kuhitimu katika shule ya Sekondari Bwawani iliyopo Mkoani Wa Pwani wakiepelekwa kujionea ujenzi wa majengo mbalimbali yanayoendelea kujengwa shule hapo yakiwemo mabweni ya wanafunzi.Picha zote na Josephat Lukaza - Lukaza Blog
Hatimaye waliowahi kusoma na kuhitimu katika Shule ya Sekondari ya Bwawani iliyopo Mkoa wa Pwani wamefanikisha adhma yao ya kuitembelea iliyokuwa shule yao kwaajili ya Kuwatia moyo na amasa vijana wanaoendelea na masomo katika shule hiyo huku wengi wao wakiwa ni vijana wa kidato cha Kwanza hadi cha Nne.

Waliowahi kuwa wanafunzi hao waliwasili majira ya saa sita mchana na kupokelewa na waliokuwa walimu wao kipindi hiko wakiwa wanasoma shule hapo na kupata nafasi ya kuonyeshwa sehemu mbalimbali za shule hiyo huku waliokuwa wanafunzi katika shule wakipata nafasi pia ya Kuzungumza machache na wanafunzi wanaoendelea na masomo katika shule hiyo na kuweza kuwasaidia vifaa vya michezo kama mipira huku wakipanda miti kwaajili ya kumbukumbu.

Waliokuwa wanafunzi wa shule hiyo inayomilikiwa na Jeshi la Magereza nchini waliweza kutoa miche 30 ya miti kwaajili ya kupandwa shule hapo huku wanafunzi wakishukuru kwa kupokea mipira kama zawadi kutoka kwa kaka na dada zao waliotangulia shuleni hapo.

Akizungumza na waliokuwa wanafunzi wa shule hiyo Kaka Mkuu msaidizi alisema "Kwa niaba ya wanafunzi wenzangu napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru kaka na dada zetu ambao mliweza kusoma hapa na kuamua kuja kutusalimia na kututia moyo, Kiukweli tumefarijika sana na tunaomba muendelea kuja shule hapa muda wowote ule kwa maana tumejisikia faraja sana kuwaona na vilevile tunapenda kushukuru kwa kutuletea Zawadi ya Mipira hii, tunasema asanteni sana"

Mara baada ya waliokuwa wanafunzi wa shule hiyo kutembelea sehemu mbalimbali za shule na kuzungumza na wanafunzi wa shuleni hapo waliweza kupata chakula cha mchana na waliokuwa walimu wao kipindi wanasoma na kuweza kubadilishana mawazo huku walimu wakishukuru sana na kusema wamefurahi sana kuwaona wanafunzi hao kwa maana ni miaka mingi sana imepita tokea wengi wao wahitimu masomo yao hapo shule.

Shule ya sekondari ya Bwawani ilikua ikiitwa Ubena kabla ya kubadilishwa jina na Kuitwa Bwawani kutokana na mantiki ya kuwa shule ya kufundisha raia peke yao ambapo awali ilikuwa ni shule kwaajili ya kuendeleza elimu kwa askari wake wa jeshi la magereza, Mnamo mwaka 2002 jina lilibadilika kutoka Shule ya Sekondari Ubena na kuitwa Bwawani ambapo sasa ilianza kupokea wanafunzi raia ambao kwa mara ya kwanza usajili wa wanafunzi raia ulianza mwaka 2001. Katika kipindi hiko shule ya Bwawani ilikuwa ni shule yenye Kidato cha Kwanza mpaka Cha nne ambapo sasa shule hiyo ina kidato cha Tano na cha sita.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)