Wafanyakazi bora Konyagi wapongezwa - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Wafanyakazi bora Konyagi wapongezwa

 Meneja idara ya  uhandisi  wa Kiwanda cha Konyagi  cha  jijini Dar es Salaam, Aranyaeli Ayo (kushoto)   akikabidhi zawadi kwa wafanyakazi  bora wa kampuni hiyo
Wafanyakazi bora wa kampuni ya Konyagi katika picha ya pamoja na Maofisa wa kampuni hiyo  muda mfupi baada ya kutunukiwa zawadi

Kampuni ya kutengeneza vinywaji ya TDL kilichopo chini ya TBL Group imewapongeza wafanyakazi wake bora katika msimu huu ambapo imewatunukia zawadi mbalimbali katika hafla iliyofanyika katika kiwanda cha Konyagi kilichopo jijini Dares Salaam

Akiongea wakati wa hafla hiyo Mkuu wa Idara ya Uhandisi wa kampuni hiyo aliwapongeza kwa kufanya kazi kwa bidii na kuongeza kuwa kampuni inathamini mchango wa kila mfanyakazi wake na ndio maana imekuwa na utaratibu wa kuwapatia tuzo mbalimbali.

Wafanyakazi hao walishukuru mwajiri wao kwa kuthamini na kutambua mchango wanaoutoa kwa kampuni

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages