Wafanyakazi bora kiwanda cha TBL Ilala wapongezwa - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Wafanyakazi bora kiwanda cha TBL Ilala wapongezwa

Meneja wa Kiwanda cha bia cha TBL Group kilichopo Ilala jijini Dar es Salaam, Calvin Martin, (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi waliofanya vizuri katika utendaji wao   wakati wa hafla ya kuwatunuku zawadi iliyofanyika  kiwandani hapo jijini Dar es Salaam.
Baadhi wafanyakazi bora waliochaguliwa na kampuni katika  kipindi hiki wakipokea zawadi mbalimbali kutoka kwa Meneja wa kiwanda cha TBL cha Dar es Salaam,Calvin Martin (kushoto) na anaeshuhudia katikati ni mtaalamu wa uzalishaji bora kwa kampuni hiyo Charles Nkondola
Kiwanda cha  bia cha TBL Group kilichopo wilayani  Ilala mkoani Dar es Salaam kimewapongeza wafanyakazi wake bora ambapo kwa kutambua mchango wao kwa kampuni kimewapatia zawadi mbalimbali katika hafla iliyofanyika kiwandani hapo mwishoni mwa wiki.
 

Meneja wa kiwanda hicho,Calvin Martin amesema kuwa kampuni inawashukuru kwa kujitoa na kufanya kazi kwa ufanisi na itaendelea kuthamini mchango wa kila mfanyakazi kwa kuwa mafanikio inaoendelea kuyapata yanatokana na mchango kwa kila mmoja wao.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages