Pages

Taswira mbalimbali za mtanange kati ya DarCity Veterans dhidi ya Boko Beach Veretans (BBV)

 Kikosi cha DarCity Veterans, kinachoongozwa na Mwanasoka wa zamani, Tippo Athuman Shaaban "Zizzou" (Wa nne kulia waliosimama) kikiwa katika picha ya pamoja, kabla ya mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Timu ya Boko Beach Veretans (BBV), uliopigwa Julai 24, 2016 kwenye Uwanja wa BBV, Boko Jijini Dar es salaam. Mchezo huo uliowakutanisha pamoja wakombwe mbali mbali wa Soka nchini enzi hizo na sasa, ulikuwa ni wa burudani ya aina yake kutokana na uwezo mkubwa wenye ufundi wa hali ya juu ulioonyeshwa na wakongwe hao, ikiwa ni sehemu ya kuwahamasisha vijana wanaochipukia na hasa wale wenye vipaji vya Mchezo wa Soka kuupenda mchezo huo na kuucheza kwa utaalam wa hali ya juu, kwani mchezo huo ni Ajira na ni burudani pia. Mchezo huo ulimalizika kwa Timu ya DarCity Veterans kuwachapa Boko Beach Veretans (BBV) Bao 3-0, Mabao mawili yakiwekwa kimiani na Mshambuliaji Machachari wa DarCity, Juma Kaseja na huku moja likitupiwa na Kiugo mchezeshaji, Salvatory Edward baada ya kupata krosi nzuri kutoka kwa Akida Makunda. Pichani toka kulia waliosimama ni Kassa Mussa, Madaraka Seleman Kibode "Mzee wa Kiminyio", Salvatory Edward, Tippo Athuman, Ally Mpemba, Maalim Chomba, Idd Seleman Kibode na Meneja wa Timu ya DarCity, Ernest Nyambo. Waliochuchumaa toka kulia ni, Akida Makunda, Macocha Moshi Tembele, Shila Mjema, Shaban Kado, Juma Kaseja, Richardson Sakala, Ally Kakima pamoja na Zubeiry Katwila.
 Kikosi cha Boko Beach Veretans (BBV) chini ya Nahodha wake Mabe (kulia waliosimama).
 Mshambuliaji wa Timu ya DarCity Veterans, Shaban Kado akiachia shuti kali kuelea langoni wa Boko Beach Veretans (BBV), huku mabeki wa timu hiyo wakiangalia namna ya kuuzuia mpira, wakati wa Mchezo wa kirafiki, uliopigwa Julai 24, 2016 kwenye Uwanja wa BBV, Boko Jijini Dar es salaam .
 Full Back wa DarCity Veterans, Ally Mpemba akiondosha hatari langoni mwao.
 Kiungo Mnyambuliko wa DarCity Veterans, Tippo Athuman Shaaban "Zizzou" akionyesha utaalam wake, katika mtanange huo wa kuvutia uliopigwa Julai 24, 2016 kwenye Uwanja wa BBV, Boko Jijini Dar es salaam .
 Mshambuliaji machachari wa DarCity Veterans, Shaban Kado akichuana vikali na mabeki wa timu ya Boko Beach Veretans (BBV), wakati wa Mchezo wa kirafiki, uliopigwa Julai 24, 2016 kwenye Uwanja wa BBV, Boko Jijini Dar es salaam .
 Akida Makunda wa DarCity Veterans, akiwa katika ubora wake, mbele ya wapinzaji wake.
 Zubeiry Katwila wa DarCity Veterans, akifanya yake.

























No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)