Pages

Tanzania yasherekea Siku ya Merit kwa kukutanisha vijana kuwapa elimu kuhusu SDGs

Katika kusherekea Siku ya Merit ambayo huadhimishwa kila Julai, 24 ya kila mwaka, vijana mbalimbali nchini wamekutanishwa kwa pamoja ili kuweza kujadili kuhusu Maendeleo Endelevu (SDGs) pamoja na kuweka mipango jambo gani lifanyike ili kuhakikisha kila raia anapata elimu kuhusu SDGs.

Akizungumza na Mo Blog kuhusu siku hiyo, Mwanaharakati wa Maendeleo Endelevu, Rose Mmbaga alisema kwa Tanzania mwaka huu wamekutanisha vijana kwa pamoja na kujadili jinsi gani wanaweza kusaidia watu wengine kujiunga katika utekelezaji wa Maendeleo Endelevu (SDGs).
Mwanaharakati wa Maendeleo Endelevu, Rose Mmbaga akitoa neno la ufunguzi katika kongamano lililokutanisha vijana ikiwa ni katika kusherekea Siku ya Merit. (Picha zote na Rabi Hume, MO Blog)

Alisema pamoja na kukutanisha vijana pia wamekutanisha mashirika mbalimbali ya ndani na nje ya nchi ambayo yataweza kuelezea jinsi gani yanafanya kazi, jinsi ambavyo yanaweza kuwasaidia vijana na jinsi ambavyo wanaweza kusaidiana na Umoja wa Mataifa (UN) ili kutekeleza Mipango ya Maendeleo Endelevu (SDGs).

"Kwa mwaka huu tumekutanisha mashirika ambayo yameungana nasi katika kuadhimisha Siku ya Merit lakini pia tuna vijana ambao wameshamaliza vyuo kwa sasa wanatafuta ajira, vijana waliomaliza kidato cha sita na wengine wamemaliza kidato cha nne," alisema Rose.
Mwanaharakati wa Maendeleo Endelevu, Rose Mmbaga akizungumza katika kongamano lililokutanisha vijana na kupata elimu kuhusu Mipango ya Maendeleo Endelevu (SDGs).

Alisema kuwa wameamua kukutanisha vijana wakiamini kuwa bado wana nguvu na wanauelewa mpana hivyo ni rahisi kwa wao kutumika kutoa elimu kwa watu wengine ambao bado hawajawa na uelewa kuhusu SDGs

Aidha alisema hiyo ni moja ya hatua za awali ambazo wanazifanya kwani wanatambua kuwa kundi kubwa la vijana bado lipo mtaani na hivyo baadhi yao wanataraji kwenda katika mkutano wa kujadili Maendeleo Endelevu (SDGs) utakaofanyika New York, Marekani na baada ya kurejea watarudi na mipango mkakati ambayo wataitumia kufikisha elimu kwa kila mtu ili ajue SDGs ni nini na jinssi gani inaweza mfikia. (Na Rabi Hume - MO Blog)
Mwanaharakati wa Maendeleo Endelevu, Rose Mmbaga akiendelea kuzungumza na vijana kuhusu SDGs.
Mwanaharakati wa Maendeleo Endelevu (SDGs), Nicolaus Mukasa akiwapa elimu washiriki kuhusu SDGs.
Baadhi ya wawakilishi wa mashirika yaliyoshiriki kongamano hilo wakielezea jinsi mashirika yao yanafanya kazi, jinsi yanavyoweza kuwasaidia vijana na kushirikiana na Umoja wa Mataifa (UN) ili kusaidia kusaidia kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs).





Baadhi ya washiriki waliohudhuria kongamano hilo.


Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)