Wafanyakazi wa TDL wakiwa na mawakala wao wakati za hafla ya uzinduzi
Meneja Masoko na Udhamini wa TBL Group,George Kavishe akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo kanda ya Kaskazini
Baadhi ya mawakala na maofisa wa TDL wakati wa uzinduzi huo
Wafanyakazi wa TDL wakiwa na mawakala wao wakati za hafla ya uzinduzi
Mawakala 2 kujishindia lori la tani 3
Kampuni ya Tanzania Distilleriers Limited (TDL) inayotengeneza na kusambaza kinywaji maarufu cha Konyagi na jamii zake, imezindua kampeni ya NUNUA, UZA, SHINDA NA KONYAGI kwa wasambazaji wa bidhaa zake kanda ya Kaskazini
Kampeni hii inawahusisha wasambazaji wa bidhaa za TDL nchini kote ilizinduliwa rasmi wiki iliyopita jijini Dar es Salaam na itadumu kwa muda wa wiki 12.
Kanda hiyo ya mauzo inajumuisha mikoa ya Arusha,Manyara,Kilimanjaro na Tanga
Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni hiyo iliyofanyika katika Hotel ya Kibo Palace mjini Arusha mwishoni mwa wiki, Meneja Masoko na Udhamini wa TBL Group,George Kavishe alisema “Dhumuni kuu la kampuni yetu ya TDL kuzindua kampeni ni kwanza kabisa kuwainua wasambazaji wa biashara zetu. Tutaweza kufikia lengo hili kwani washindi wa kampeni hii watajishidia magari mapya mawili ya usambazaji (Eicher 3 Tonne Truck). Tunaamini kwa magari haya wasambazaji wetu wataweza kurahisishwa utendaji wao ndani ya maeneo yao ya mauzo”
Pia, kupitia shindano hili tutaweza kuchangia maendeleo ya kichumi nchini pamoja na jamii kwa ujumla. Aliendelea kusema.
Bwana Kavishe alisema katika shindano hili wasambazaji wa bidhaa za TDL wamewekewa viwango vya mauzo; na washiriki wote watakaofikia vigezo wataingia kwenye droo kubwa ya kupata mshindi itakayofanyika mwanzoni mwa mwezi wa 10. “Tunaamini kabisa kampeni hii itaongeza ufanisi kwa wasambazaji wetu nao wataongezea chachu ya manunuzi ya bidhaa zetu”.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)