Pages

Nini maoni juu ya IMF kutoa onyo kwa Tanzania?

Hii ni sehemu ya Habari kwenye Gazeti la The Guardian Katika Ukurasa wa Kwanza ambapo Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) limeionya Serikali ya Tanzania kuwa makini na tabia yake ya kuwekeza katika Miundo Mbinu

Ikumbukwe hapo jana Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli alikutana na Rais wa Benki ya Exim ya China Liu Liang , Ikulu Ndogo Chamwino Mkoani Dodoma ambapo moja ya mambo waliyoongelea ni Kuhusu Benki hiyo ya Exim ya China kuipatia Mkopo wa masharti nafuu Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kiasi cha Dola za Kimarekani Bilioni 7.6 ambazo sawa na zaidi ya Shilingi za Kitanzania Trilioni 16 kwaajili ya kugharamia ujenzi wa mradi mkubwa wa reli ya kati hapa nchini katika kiwango cha kisasa (Standard Gauge) unaotarajiwa kuanza katika mwaka huu wa fedha.

Je nini Maoni yako kuhusiana na IMF kutoa onyo hilo kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania? Tupate maoni yako nasi tutayapachika hapa 

Kwa habari ya Rais wa Benki ya Exim ya China na Rais wa Tanznaia, Dkt John Pombe Magufuli SOMA HAPA

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)