Pages

Dk. Kigwangalla amaliza ziara yake ya kuwashukuru Wananchi wa Jimbo la Nzega Vijijini

Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla amemaliza ziara yake ya kuwashukuru Wanachi wa Jimbo hilo kwa kumchagua kuwa Mbunge wao huku akiwaahidi kuendelea kushirikiana nao katika shughuli za kimaendeleo kama alivyotoa ahadi katika uchaguzi uliopita.

Katika ziara hiyo iliyoanza Julai 13 na kufikia tamati Julai 20, mwaka huu, Dk. Kigwangalla ameweza kuzunguka Vijiji mbalimbali vilivyo katika Kata 19 za Jimbo hilo ambapo amekutana na wananchi hao na kutoa shukrani zake.

Dk. Kigwangalla katika ziara hiyo, amewaomba Wananchi wa Jimbo hilo waendelee kumuombea kwani kazi ndio imeanza na kuwataka wananchi hao kushirikiana nae bega kwa bega katika shughuli za kimaendeleo.

“Kwanza nashukuru kwa kura zenu. Hakika zilitosha kuniwezesha mimi kuwa Mbunge. Kwa kura zenu nyingi pia zimewezesha kumpata Rais wetu Dk. Magufuli na Madiwani wengi katika Jimmbo hili. Nawashukuru sana Wana Nzega Vijijini” alieleza Dk. Kigwangalla.

Aidha, Dk. Kigwangalla katika ziara hiyo, alipata wasaha wa kutembelea maeneo mbalimbali ikiwemo sehemu za shule, Vituo vya Afya ambapo alijioenea hali ilivyo huku akieleza kuwa ataendelea kushirikiana na Watendaji wote wa ngazi ya Kijiji, Kata na ngazi za juu.

Dk. Kigwangalla pia aliweza kutoa misaada ya vifaa vya michezo kwa vijana mbalimbali ambapo awali aliwaahidi yeye mwenyewe.

Kata zinazounda Jimbo hilo la Nzega Vijijini ni pamoja na Kata ya Puge, Ndala, Nata,, Sanzu, Lusu, Milambo Itobo, Magengati, Budushi, Nkiniziwa, Mbagwa, Mizibaziba, Utwigu, Muhugi, Mwantundu, Wela, Mwasala, Tongi, Ugembe na Mwakanshanhala.

Aidha, Dk.Kigwangalla alipata wasaha wa kushiriki mazishi ya Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdalla Simba ambaye alikuwa mwenyekiti wa CCM Kata wa Nzega Magharibi aliyefariki Julai 19 jioni.

Marehemu Mzee Simba ambaye alikuwa mkongwe kwenye chama hicho tokea chama cha TANU ambapo aliwelezewa kuwa alikuwa mstari wa mbele katika kukiunganisha chama cha TANU na baadae CCM.

Mpaka umahuti unamkuta alikuwa Mwenyekiti wa CCM wa tawi hilo. Dk. Kigwangalla pia alipata kutoa ubani na kuwajulia pole ndugu wa wafiwa.
U36-620x399 DSC_2426Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akiingia kucheza sambamba na vijana wa Sungusungu wa Jadi
DSC_2442
Vijana wa Sungusungu wakicheza ngoma za jadi wakimuonyesha mgeni Dk. Kigwangalla ambaye ni Mbunge wa Jimbo hilo la Nzega Vijijini
DSC_2459 DSC_2419 DSC_2482
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akipiga picha ya pamoja na vijana wa Sungusungu wa jadi waliokuwa wakitoa burudani
DSC_2670
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa vifaa vya michezo kwa mmoja wa viongozi wa timu ya Lusu (Kata ya Lusu)
DSC_2585 DSC_2536 DSC_2614
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akipata picha yaa pamoja
DSC_2541 DSC_2621 DSC_2423
Vijana wa Sungusungu wakifanya mambo..
DSC_2492 DSC_2838Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na walimu katika shule ya Msingi Nata
DSC_2860 DSC_2862
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akisaini kitabu cha wageni cha shule ya Msingi Nata
DSC_2863
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Nata
DSC_2796 DSC_2876 DSC_2881
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akiwahutubia Wananchi wa Kata ya Nata.
DSC_2528 DSC_2536 DSC_2496
Vijana wa Sungusungu wakifuatilia mkutano huo wa Dk. Kigwangalla (hayupo pichani).
DSC_2519 DSC_2568
Vijana wa Sungusungu wakitoa budani katika mkutano huo wa Dk. Kigwangalla (Hayupo pichani). Picha zote na Andrew Chale, Nzega).

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)