Pages

NAIBU WAZIRI WA KAZI, VIJANA NA AJIRA AFUNGUA KONGAMANO KUBWA LA VIJANA MKOANI MWANZA.

Mgeni Rasmi, Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini mkoani Dodoma, Mhe.Antony Peter Mavunde, akizungumza katika ufunguzi wa Kongamano la Vijana Wajasiriamali na Wawekezaji mkoani Mwanza.

Kongamano hilo ambalo limeandaliwa kwa ushirikiano wa pamoja kati ya taasisi ya "Tanzania Youth Enterpreneurship Organization-TAYEO) pamoja na Vijana Mwanza Saccos, linafanyika katika viwanja wa Gandh Hall Jijini Mwanza kwa siku mbili, leo Julai 16,2016 hadi kesho Julai 17,2016 ambapo mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nhauye.

Wadau mbalimbali wa maendeleo wakiwemo taasisi ya Desk and Chair Foundation, Mfuko wa Hifadhi ya jamii PPF, Kampuni ya mafuta ya Petro Africa, Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Ofisi ya mbunge wa jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula, Ofisi ya mbunge wa jimbo la Ilemela, Mhe.Angelina Mabula ambae pia ni Naibu waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, City Fm na Mhe.Jumanne Kishimba ambae ni mbunge wa jimbo la Kahama Mjini.
Na BMG
Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe.Antony Mavunde (kushoto) pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Kongamano (kulia), wakifurahia jambo katika kongamano hilo.
Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Kiomoni Kiburwa Kibamba, akizungumza katika kongamano hilo.
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula (kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Kiomoni Kiburwa Kibamba (kulia), wakifuatilia kongamano hilo.
Flora Magabe, akisoma Risala kwa niaba ya waandaaji wa Kongamano hilo.
Viongozi pamoja na wadau mbalimbali wakiwa katika kongamano hilo.
Waandaaji wa Kongamano la Vijana Wajasiriamali na Wawekezaji mkoani Mwanza
Mwenyekiti wa Shirika la Machinga mkoani Mwanza (katikati) akiwa pamoja na wadau wengine katika Kongamano la Vijana Wajasiriamali na Wawekezaji mkoani Mwanza.
Wadau mbalimmbali wakiwa katika Kongamano la Vijana Wajasiriamali na Wawekezaji mkoani Mwanza.
Wadau mbalimmbali wakiwa katika Kongamano la Vijana Wajasiriamali na Wawekezaji mkoani Mwanza.


Vijana mkoani Mwanza wameaswa kutambua fursa za kiuchumi zilizopo kwenye maeneo yao na kuzitumia kikamilifu ili kupambana na uhaba wa ajira unaosababisha kukithiri kwa umasikini katika jamii.


Akifungua hii leo kongamano la siku mbili la vijana kutoka wilaya zote saba za mkoa wa Mwanza, Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde, amesema mkoa wa Mwanza unazo fursa nyingi za kiuchumi ikiwemo ardhi kwa ajili ya kilimo na Ziwa Victoria kwa ajili ya uvuvi,hivyo vijana wanapaswa kuzitumia ipasavyo fursa hizo.


Amesema kumejengeka tabia miongoni mwa vijana kulalamikia uhaba wa ajira jambo ambalo amesema linasababishwa na vijana hao kushindwa kujitambua huku wengine hasusani wanaohitimu vyuo vikuu wakichagua kazi za kufanya hivyo kuongeza idadi ya vijana wasio na ajira mitaani.



Aidha Naibu Waziri Mavunde amezitaka Halmashuri zote nchini kuhakikisha zinatenga asilimia tano ya fedha za mapato mbalimbali kwa ajili ya kuwawezesha vijana huku pia akiwaagiza wakuu wa mikoa, wilaya na wakurugenzi wa Halmashuri kutenga maeneo kwa ajili ya vijana na


akina mama kufanya biashara zao bila kubughudhiwa.


Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba, amesema Halmashauri ya jiji hilo itahakikisha inatenga asilimia tano ya mapato yake kwa ajili ya vijana na akina mama huku akiwataka vijana kuhamasisha wananchi kulipa kodi ili fedha hizo zipatikane.


Awali akisoma risala kwa niaba ya waandaali wa kongamano hilo, Flora Magabe, amesema vijana wa mkoa wa Mwanza wamepanga kuwekeza kwenye kilimo na ufugaji wa kuku na kuiomba serikali kuwapatia maeneo kwa ajili ya kuendesha miradi hiyo.

Kongamano la Vijana Wajasiriamali na Wawekezaji mkoani Mwanza, limeandaliwa kwa ushirikiano wa pamoja kati ya taasisi ya Vijana Wajasiriamali Tanzania (Tanzania Youth Enterpreneurship Organization-TAYEO) pamoja na Chama cha Akiba na Mikopo cha Vijana Mwanza Saccos, ambapo linafanyika katika viwanja wa Gandh Hall Jijini Mwanza, leo na kesho.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)