Mtafiti wa kimataifa wa Sokwe mtu na Mwanaharakati wa haki za Wanyama,Dkt Jane Goodall akielekea katika msitu wa Hifadhi ya Taifa ya Gombe kwa ajili ya mahojiano maalumu na wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari vya Tanzania.
Mtafiti Dkt Jane Goodall akichukua taswira mara baada ya kuona kundi la Wanahabari katika msitu wa Hifadhi ya Taifa ya Gombe wakimngojea.
Mtalii raia wa Colombia ,Sandra Renasco akihamaki baada ya kuonana ana kwa ana na Dkt Jane Goodall ,mtu ambaye anamtaja kama Role Model wake.
Mtafiti wa Kimataifa wa Sokwe ,Dt Jane Goodall akisalimiana na Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete baada ya kukutana katika Hifadhi ya Taifa ya Gombe. katikati ni Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya taifa ya Gombe ,Dkt Noelia Muyonga na kulia ni mwanahabari Mkinga Mkinga.
Mtafiti ,Dkt Jane Goodall akimueleza jambo Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa Pascal Shelutete kabla ya kuanza mahojiano na waandishi wa habari.kushoto mwa Dkt Goodall ni Daktari wa mifugo Dkt ,Anthony Collins .
Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa ,(TANAPA) Pascal Shelutete akifanya utamburisho wa Wanahabari waliofika katika Hifadhi ya Taifa ya Gombe kwa ajili ya mahojiano na Dkt Jane Goodall.
Mtafiti wa Kimataifa wa Sokwe Dkt Jane Goodall akijibu maswali ya wanahabri (hawapo pichani) wakati wa mahojiano maalumu yaliyofanyika katika Hifadhi ya Taifa ya Gombe.
Dkt Jane Goodall akionesha namna ambavyo amewazoesha Sokwe waliopo katika Hifadhi ya Taifa ya Gombe kusalimiana ,mwingine hapo ni mwanahabari Mkinga Mkinga.
Dkt Goodall akiwa katika picha ya pamoja na Wanahabri mara baada ya kumaliza mahojiano.
Dkt Goodall akiwa katika picha ya pamoja na Watalii kutoka nchini Colombia.
Dkt Jane Goodall akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi katika Hifadhi ya Taifa ya Gombe iliyoko mkoani Kigoma.
Na Dixon Busagaga Kigoma.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)