
Kutoka kushoto ni Meneja wa Huawei nchini Tanzania Bw. Huxiangyang Jacko akifuatiwa na Mkuu wa Kitengo cha Mauzo na usambazaji Vodacom Tanzania George Rwehumbiza, Mkurugenzi wa mauzo na Usambazaji wa Huawei Tanzania Bwana Sylvester Manyara na mwisho ni Bw. Edwin Byampanju meneja bidhaa kutoka Vodacom wakionyesha kipeperush cha simu mpya ya Huawei kishkwambi wakiwa mara baada ya mkutano na waandishi wa habari katika uzinduzi wa simu hiyo inayokuja na ofa kabambe kutoka Vodacom, uliofanyika katika ukumbi wa Western Coral Beach Hotel, jijini Dar es Salaam
Uongozi wa kampuni ya Huawei Device Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Vidacom Tanzania mara baada ya mkutano na waandishi wa habari katika uzinduzi wa simu mpya ya Huawei kishkwambi inayokuja na ofa kabambe kutoka Vodacom, uliofanyika katika ukumbi wa Western Coral Beach Hotel, jijini Dar es Salaam

Kushoto ni Meneja wa Huawei nchini Tanzania Bw. Huxiangyang Jacko akiongea na waandishi wa habari katika uzinduzi wa simu mpya ya Huawei kishkwambi inayokuja na ofa kabambe kutoka Vodacom, uliofanyika katika ukumbi wa Western Coral Beach Hotel, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mauzo na usambazaji Vodacom Tanzania Bw. George Rwehumbiza
Meneja wa Huawei nchini Tanzania Bw. Huxiangyang Jacko akitoa hotuba kwenye mkutano na waandishi wa habari katika uzinduzi simu mpya ya Huawei kishkwambi inayokuja na ofa kabambe kutoka Vodacom. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mauzo na usambazaji Vodacom Tanzania George Rwehumbiza na Mkurugenzi wa mauzo na Usambazaji wa Huawei Tanzania Bwana Sylvester Manyara
Meneja wa Huawei nchini Tanzania Bw. Huxiangyang Jacko akitoa hotuba kwenye mkutano na waandishi wa habari katika uzinduzi simu mpya ya Huawei kishkwambi inayokuja na ofa kabambe kutoka Vodacom. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mauzo na usambazaji Vodacom Tanzania George Rwehumbiza na Mkurugenzi wa mauzo na Usambazaji wa Huawei Tanzania Bwana Sylvester Manyara
Mkuu wa Kitengo cha Mauzo na usambazaji Vodacom Tanzania George Rwehumbiza akitoa hotuba kwenye mkutano na waandishi wa habari katika uzinduzi simu mpya ya Huawei kishkwambi inayokuja na ofa kabambe kutoka Vodacom. Kushoto ni Meneja wa Huawei nchini Tanzania Bw. Huxiangyang Jacko na Kulia ni Mkurugenzi wa mauzo na Usambazaji wa Huawei Tanzania Bwana Sylvester Manyara

Mkurugenzi wa mauzo na Usambazaji wa Huawei Tanzania Bwana Sylvester Manyara akiongea na waandishi wa habari kwenye mkutano na waandishi wa habari katika uzinduzi simu mpya ya Huawei kishkwambi inayokuja na ofa kabambe kutoka Vodacom.
Dar es Salaam Julai
2016. Katika mwendelezo wa kuhakikisha kuwa
watanzania wanapata haki yao ya mawasiliano na kumiliki sio simu tu bali simu
ya kisasa, Huawei imeendelea kuchanja mbuga katika kujiongezea soko la simu
zake nchini na kuongeza bidii kuingiza simu bora za kisasa zenye gharama nafuu.
Katika moja ya mpango wao wa kibunifu katika kuleta chaguo bora kwa wanunuzi wa
simu wanaohitaji kupata simu bora na kwa gharama nafuu, Huawei imeshirikiana na
Vodacom Tanzania kuleta simu ya Huawei Kishkwambi iliyounganishwa na kifurushi
cha Vodacom cha muda wa maongezi na internet.
Promosheni ya Huawei Kishkwambi inaenda sambamba na uzinduzi wa
maonyesho ya kimataifa ya biashara ya Saba Saba. Simu hii inanunuliwa kwa sh.
100,000 tu, ikiwa na kifurusha cha bure cha internet cha GB6 na dakika 100 za
bure za maongezi katika mtandao wa 3G wa Vodacom kwa mwaka mmoja. Simu hii pia
huja na waranti ya miezi 12 kutoka Huawei.
Katika juhudi zake za kuongeza idadi ya watumiaji wa simu za kisasa
nchini Tanzania, Huawei imeona haja ya kuwawezesha watumiaji wa simu kuwa na
chaguo bora la kununua simu halisi. Mara baada ya kuanza kwa utaratibu wa
kuzima simu feki, simu nyingi sana zimezimwa
na wengi wa watumiaji ambao walijibana ili kumudu kununua simu za gharama nafuu
sasa hawana tena simu. Promosheni hii ni fursa adhimu kwa watumiaji ili kununua
si tu simu mpya bali pia simu ambayo inaweza kuwa na data za internet, simu
orijino, yenye waranti ya miezi 12 lakini pia ya gharama nafuu sana.
Mkurugenzi Mkazi wa Huawei Bw. Huxiangyang Jacko anasema, “Huawei
imedhamiria kufikia maeneo yote ya soko la Tanzania kupitia bidhaa zao nyingi
ambazo pia zimethibitika kufanya vema katika masoko mengine ulimwenguni. Lakini
kwa Tanzania, tunataka kuweka mkazo kwa watu wa kipato cha kati na cha chini,
wanafunzi na wafanyakazi vijana ambao wanathamini ubora na pia wanajali bei.
Kwa sababu hiyo, Huawei Kishkwambi inaonesha kuwa ndio simu bora tunayoweza
kuwapatia wateja wetu ambayo yaweza kuwa ndio simu ya kwanza au pia kwa wale
wanaotaka kuongeza simu ya pili”.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Mkuu wa Kitengo cha
Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania, Bw. George Rwehumbiza alisema
ushirikiano wao na Huawei unaendana na nia ya Vodacom Tanzania ya kuwapatia
wateja wao fursa ya kununua simu bora na za bei nafuu hususani baada ya zoezi
la hivi karibuni la uzimaji simu feki lililotekelezwa na TCRA.
“Vodacom Tanzania imekuwa mstari
wa mbele kuhakikisha kuwa wateja wake wanaendelea kuunganishwa hata baada ya
uzimaji mkubwa wa simu uliofanywa na TCRA, hivyo basi ushirikiano wetu na
Huawei unaongeza msukumo wetu kuhakikisha kuwa wateja wetu wanabakia wakiwa
wameunganishwa na katika hilo pia tunawapatia motisha ya vifurushi vya internet
na muda wa maongezi lukuki” alisema afisa huyo wa Vodacom Tanzania.
Huawei Kishkwambi ni simu iliyowezeshwa kwa 3G na inazo sifa zote za
simu za kisasa, na kwa vifurushi vya gharama nafuu vya muda wa maongezi na
internet wateja wanaweza kuperuzi mtandaoni, Facebook na hata Instagram. Simu
hii ina kioo cha LCD cha inchi 4. Ili kuleta mvuto wa kipekee, Huawei
Kishkwambi ina mgongo wenye mkunjo kwa mbali na kona zake nne zilizopinda bila
ncha kali. Muundo wake huu wa kipekee
unawapa watumiaji wake hisia nzuri wanapoishika na ni rahisi kuitumia hata kwa
mkono mmoja. Ina megapikseli 0.3 katika kamera yake ya mbele na megapikseli 2
katika kamera ya nyuma. Huawei Kishkwambi ina prosesa 2 ambazo huipa uwezo wa
kufanya kazi haraka sana katika kucheza michezo ya kwenye simu (game). Kadi
yake ina ukubwa wa MB512 na ROM ya GB4 ambayo inaweza kuongezwa kwa kadi ya
nje. Simu hii ina spidi ya hali ya juu na uwezo mkubwa wa kutunza chaji.
Ushirikiano huu wa kipekee wa miamba miwili ya kimataifa nchini Tanzania
ni hatua ya kimkakati ya Huawei na Vodacom ya pamoja katika kuleta suluhisho
kwa watumiaji wa simu. Kila simu ya kisasa inahitaji kuunganishwa na mtandao
bora ili kuleta ubora halisi kwa mtumiaji wa simu. Hapa ndipo utendaji wa simu
ya Huawei Kishkwambi unapoendana na mtandao wenye kasi wa Vodacom 3G kuleta
nguvu Zaidi kwa watumiaji.
Katika kufanikisha wazo la serikali kuwa haki ya kuwasiliana inapaswa
kumfikia kila mtanzania, Vodacom imekuwa ikifanya jitihada pasipo kuchoka
katika kuwaunganisha watanzania na kuongeza uwekezaji katika sekta ya
mawasiliano ya simu. Ushirikiano na Huawei katika promosheni ya Huawei
Kishkwambi ni moja ya namna nyingi ya ofa zinazotolewa kwa wateja. Promosheni
hii maalum ya Huawei Kishkwambi inatolewa katika maduka yote ya Huawei na
Vodacom nchini kote. Huawei na Vodacom kwa pamoja zinawahimiza watanzania
kuitumia vilivyo fursa ya promosheni hii na kufurahia kuendelea kuunganishwa
kimawasiliano.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)