Meneja wa Mazingira wa SABMiller atembelea Wizara ya Maji na Umwagiliaji - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Meneja wa Mazingira wa SABMiller atembelea Wizara ya Maji na Umwagiliaji

 Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Mhandisi   Mbogo Futakamba,( kulia)akimsikiliza kwa makini  Meneja mazingira wa SABMiller  Muzi Chonco)  wakati alipofanya ziara ya kikazi ofisini kwake Ubungo jijini Dar es Salaam,  (Kushoto) ni Meneja wa  kiwanda cha bia cha TBL Group   Ilala Dar es Salaam Bw. Calvin Martin



Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Mhandisi   Mbogo Futakamba,(wa pili kutokea kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Meneja Mazingira wa SABMiller na Maofisa wa TBL Group walipomtembelea ofisini kwake mwishoni mwa wiki


Meneja anayeshughulika na masuala ya Mazingira wa kampuni ya vinywaji ya SABMiller kanda ya Afrika,Bw.Muzi Chonco,ambaye yuko nchini kwa ziara ya kikazi mwishoni mwa wiki alifanya ziara katika Wizara ya Maji na Umwagiliaji ambapo alikukutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhandisi Mbogo Futakamba.
Bw.Chonco katika mazungumzo hayo aliweza kumweleza Katibu Mkuu  miongozo na mikakati mbalimbali ya kampuni hiyo kuhusiana na utunzaji wa mazingira,matumizi sahihi ya maji ,utunzaji wa vya maji na miradi ambayo kampuni inasaidia kuendesha.
Kampuni ya SABMiller  kwa hapa nchini inamiliki kampuni ya kutengeneza vinywaji ya TBL Group ambayo inamiliki viwanda  mbalimbali vya kutengeneza vinywaji hapa nchini.
Katika ziara hiyo ya kikazi Bw.Chonco aliongozana na Meneja wa kiwanda cha kutengeneza bia cha TBL kilichopo Ilala jijini Dar es Salaam,Bw.Calvin Martin na maofisa wengine wa kampuni ya TBL Group.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages