KYERWA NA BIHARAMULO KUANZA UTEKELEZAJI AWAMU YA KWANZA YA MRADI WA PS3 MKOANI KAGERA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

demo-image

KYERWA NA BIHARAMULO KUANZA UTEKELEZAJI AWAMU YA KWANZA YA MRADI WA PS3 MKOANI KAGERA

DSC_0500
Kiongozi wa Timu ya Uzinduzi wa Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) mkoani Kagera, Abdul Kitula (kulia) akimkabidhi bahasha iliyo na majina ya Halmashauri mbili zilizopitishwa kuanza utekelezaji wa mradi wa PS3, Katibu Tawala Mkoa wa Kagera, Amantius Casmiri Msole mjini Bukoba leo. Halmashauri Mbili za Wilaya ya Kyerwa na Biharamulo ndizo zimechaguliwa kuanza utekelezaji wa mradi huo.
DSC_0495
 Katibu Tawala Mkoa wa Kagera, Amantius Casmiri Msole akionesha bahasha hiyo iliyo na majina.
DSC_0497
Katibu Tawala Mkoa wa Kagera, Amantius Casmiri Msoleakizisoma Haklamashauri zilizo chaguliwa ambazo ni   Wilaya ya Kyerwa na Biharamuloambazo zimeonekana kuwa na uhitaji mkubwa wa kuimarisha mifumo yake kulinganisha na Halmashauri zingine sita za Karagwe, Muleba, Misenyi, Ngara, Bukoba Mji na Bukoba ambazo zitaingia awamu ya pili.
DSC_0482
 Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, Col (Mstaafu) Shaban Shaban Ilangu Lissu ambaye Wilaya yake imechaguliwa kuanza awamu ya kwanza ya utekelezaji wa mradi wa PS3.
DSC_0493
 Ofisa kutoka PS3 Soud Abubakar akiwasilisha sifa na vigezo vilivyo tumika kuzipata Halamashauri mbili za awali zilivyo patikana ili ziweze kuanza utekelezaji wa mradi.
DSC_0391
 Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Kigoma wakifuatilia uwasilishaji wa taarifa kutoka Wilaya mbalimbali.
DSC_0393
 Washiriki wakifuatilia uwasilishajki huo.
DSC_0390
Mwakilishi wa Halmashauri ya Mji wa Bukoba, ambaye ni Mchumi Msaidizi, Rahel Mbuta akiwasilisha kazi za makundi ambazo ziliainisha Changamato na maeneo ya uboreshaji. 
DSC_0412
 Meneja wa Mifumo ya Habari na Mawasiliano wa Mradi wa PS3, Giovvan Di Piazza akiwajibika kuhakikisha mawasilisho yote yanaenda vyema.
DSC_0420
 Washiriki wakifuatilia uwasilishaji kutoka katika makundi.
DSC_0405

Mwakilishi wa Halmashauri ya Wilaya wa Bukoba, ambaye ni Mhandisi wa Maji, Ndolimana Kijigo akiwasilisha kazi za makundi ambazo ziliainisha Changamato na maeneo ya uboreshaji.
DSC_0443
 Washiriki wakiwamakini kusikiliza mada
DSC_0439
Mkaguzi wa Hesabu wa Ndani wa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi, Imani Mgonja akiwasilisha tarifa ya kundi la Halamashauri yake.
DSC_0455
 Maofisa kutoka Wizarani wakifuatilia kwa makini mawasilisho hayo.
DSC_0424
 Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba, Henrietta William akiwakilisha Halmashauri yake.
DSC_0448 
Mmoja wa washiriki akiuliza swali kutokana na mawasilisho ya makundi mbalimbali.

DSC_0463Mratibu wa Mradi wa PS3 kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Bertha Swai akijibu na kutolea ufafanuzi baadhi ya maswali yaliyoulizwa na washiriki.
DSC_0466
 Ofisa Utumishi kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Debora Mkemwa akifafanua baadhi ya hoja.
DSC_0470
Dk Rest Lasway (kushoto) akizungmza na Nanzia Florence wote kutoka PS3.
DSC_0478
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuu kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Sebastian Kitiku akichangia na kujibu hoja zilizotolewa.
DSC_0509
 Mtaalam wa fedha wa PS3 ambaye pia ni Kiongozi wa Uzinduzi wa mradi Mkoa wa Kagera, Abdul Kitula akizungumza.
DSC_0513
 Mtaalam wa Masuala ya Utawala Bora katika Mradi wa PS3, Paul Chikira akizungumza kwa niaba ya timu nzima ya PS3 iliyopo mkoani Kagera.
DSC_0517Wenyeviti wa Halamashauri za Wilaya za Biharamulo, Hafsa Galiatano na Mwenzake kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa, Kashunju Runyogote wakisikiliza utangazaji wa Halmashauri zinazoanza mradi ambapo Halmashauri zao zimechaguliwa kuanza. Source:Father Kidevu Blog

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Pages