Wafanyakazi wa TBL Group katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi huo
Meneja masoko na Udhamini wa TBL Group,George Kavishe akizungumza na wadau na wasambazaji (hawapo) wa vileo aina ya konyagi kwenye ukumbi wa Hotel ya Beaco Jijini Mbeya.
Baadhi ya wasambazaji kutoka mikoa ya Nyanda za Juu Kusini walishiriki uzinduzi wa Kampeni ya Nunua, Uza Shinda ya Konyagi kwenye Hotel ya Beaco Jijini Mbeya
-Lori 2 kutolewa kwa washindi
Kampuni ya Tanzania Distilleriers Limited (TDL) inayotengeneza na kusambaza kinywaji maarufu cha Konyagi na jamii zake, imezindua kampeni ya NUNUA, UZA, SHINDA NA KONYAGI kwa wasambazaji wa bidhaa zake kanda ya Nyanda za juu itakayodumu kwa muda wa wiki 12.
Kanda hiyo ya mauzo inajumuisha mikoa ya Mbeya,Iringa,na mikoa ya Kusini mwa Tanzania
Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni hiyo iliyofanyika katika Hotel ya Beaco mjini Mbeya jana , Meneja Masoko na Udhamini wa TBL Group,George Kavishe alisema “Dhumuni kuu la kampuni yetu ya TDL kuzindua kampeni ni kuwainua wasambazaji wa biashara zetu. Katika kufanikisha suala hili wasambazaji wetu 2 watakaoibuka kila mmoja atajishindia lori jipya la usambazaji vinywaji aina ya Eicher lenye uzito wa tani 3”.
Pia alisema kuwa wasambazaji wa bidhaa za kampuni wataweza kujishindia zawadi mbalimbali katika kipindi hiki cha kampeni lengo kubwa ni kuwawezesha kufanya biashara zao kwa ufanisi na kuongeza mapato yao ikiwemo kuchangia maendeleo ya kichumi nchini pamoja na jamii kwa ujumla.
Bwana Kavishe alisema katika shindano hili wasambazaji wa bidhaa za TDL wamewekewa viwango vya mauzo; na washiriki wote watakaofikia vigezo wataingia kwenye droo kubwa ya kupata mshindi itakayofanyika mwanzoni mwa mwezi wa 10. “Tunaamini kabisa kampeni hii itaongeza ufanisi kwa wasambazaji wetu nao wataongezea chachu ya manunuzi ya bidhaa zetu”.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)