Dar
es Salaam, Julai 2016;.
Kampuni ya Huawei wakishirikiana na makampuni ya mtandao wa simu Vodacom,
Airtel na Tigo wamezindua promosheni kwa ajili ya wananchi wote watakaohudhuria
maonyesho ya Saba Saba katika matoleo
yake ya simu za kisasa za Y3II, Y3 C, na toleo mahususi la Y3 Lite. Katika
maonyesho hayo, wananchi wataweza kujipatia simu mpya halisi kwa bei rahisi
zaidi
Tukizingatia kwamba kila Mtanzania
anayo haki ya kuendelea kuunganishwa na ndugu, jamaa na marafiki kwa njia ya
mawasiliano ya simu bila kujali tofauti zao za kipato, Huawei kwa mara nyingine
inafanikisha hilo kwa kuleta simu zake za
Yseries ili kuwezesha upatikanaji wa
simu za kisasa za gharama nafuu kwa watumiaji wa simu wa kipato cha chini
Tanzania.
Huawei
Tanzania kwa kupitia mkakati wake huu wa kushirikiana na makampuni ya
mawasiliano; Tigo, Vodacom na Airtel inampa mtumiaji fursa ya kugusa, kuhisi na
kufurahia namna za kipekee za utendaji wa matoleo haya ya Y series ikiwamo Y3II, Y3Lite, Y3 C na Y6 Pro.
Akizungumzia kuhusu ofa na punguzo hili la simu, Meneja Masoko wa Huawei
Tanzania Bi. Jane Wang amewahimiza wananchi wote watakaofika katika maonyesho
ya Saba Saba kutembelea mabanda ya Vodacom, Tigo na Airtel katika viwanja vya
Mwalimu Nyerere kuanzia tar 28 June mpaka tar 8 Julai ili kujipatia moja ya
hayo matolea ya simu za Huawei.”Ofa ya
Huawei na Vodacom ni katika simu ya Huawei Kishkwambi kwa gharama y ash.
100,000 ambapo mteja atajipatia kifurushi cha bure cha dakika 1000 na interent
GB6 kwa muda wa miezi 12.” Alisema.
Promosheni
ya Huawei na Tigo huwawezesha wateja kununua simu ya Huawei Y3 Lite kw ash.
125,000 tu, ikiwa na kifurushi cha GB 2 za data pamoja na muda wa maongezi wa
thamani ya sh. 10,000 kwa muda wa miezi 6. Kwa Y3II Tigo inatoa ofa ya GB 10 na
dakika 3000 kwa kupiga Tigo – Tigo na dakika 500 kupiga mitandao mingine kwa
muda wa miezi 3. Y3 C inakuja na dakika 100 za kupiga mitandao yote, kifurushi
cha internet cha GB1 na sms 10,000 kwa miezi 4 kutoka Airtel”
Akizungumzia
kuhusu simu za gharama ya chini na uhitaji wake kwa watu wa kipato cha chini,
Mkurugenzi wa Mauzo wa Huawei Tanzania, Bw. Sylvester Manyara alisema,
ukiziangalia simu hizi ni vigumu kuamini kuwa ni simu za gharama ya chini kwa
sababu simu zote zimeundwa kwa muundo na teknolojia ya hali ya juu na ya
kimataifa. Y3 Lite inafaa Zaidi kwa ajili ya watu wazima, wanafunzi na watu wa
kipato cha kati na cha chini ambao kwao gharama na utendaji wa simu huwa na
umuhimu sawia. Simu hii inawafaa wale ambao wanahitaji kuitumia simu kwa muda
mrefu sana bila kuichaji. Ni moja ya simu pekee katika zenye thamani hii
zinazoweza kuvumilia matumizi makubwa. Betri yenye uwezo mkubwa ya Huawei Y3
Lite inayohifadhi nguvu kwa kiwango cha juu inaiwezesha simu hii kudumu na
chaji kwa zaidi ya siku nzima.
Simu ya
Huawei Y3 Lite ina kamera yenye uwezo maradufu wa megapikseli 2 katika kamera
yake ya mbele na megapikseli 5 ukilinganisha na hizi zingine, ambazo kamera
yake ya mbele kwa kawaida ni megapikseli 0.8 na ya nyuma ni megapikseli 2 na taa
mbili za kamera ambazo huwezesha mwonekano mzuri wa picha hasa zinazopigwa
katika mazingira yenye giza. Simu ya
Huawei Y3 Lite ina uwezo mkubwa wa kupiga na kuboresha picha na sauti.
Huawei Y3II
si tu ni simu yenye teknologia ya juu, lakini pia inamwoneka wa kipekee pia.
Simu hii huja na aina tofauti za mtindo wa rangi. Huawei Y3II inayo kasi kubwa
ya kushusha mafaili au picha kwa kasi inayofikia hao MB 21 kwa dakika
inayowaezesha watumiaji kuperuzi kurasa za Facebook, Instagram na Whatsapp kwa
haraka. Kwa mujibu wa Bw. Manyara, simu ya Y3 II imekusudiwa kwa ajili ya
watanzania wa kipato cha chini kabisa na cha kati ambao huhitaji kufurahia
maisha, lakini pia hujali kuhusu gharama huku wakihitaji bidhaa bora, ya
gharama nafuu na inayodumu.
“Kwa mujibu wa tafiti zetu, vijana wa kisasa
hupenda hupenda kusikiliza muziki kwa sauti na kujivinjari na marafiki.Y3II
inaokoa muda kwa kuweza kupangilia njia za mkato za kwa matumizi kwa kufuata
hatua tatu tu rahisi kama vile, kubofya, kubofya mara mbili, au kubofya kwa
muda”. Alisema Bw. Manyara.
Akiyazungumzia matoleo ya Huawei Y
Meneja wa Huawei nchini Tanzania Bw. Huxiangyang Jacko amethibitisha kuwa
Huawei wanazo bidhaa sahihi kwa kila aina ya mteja, ikijumuisha teknologia ya
kiwango cha juu, ubunifu, utendaji mzuri na mwonekano bora kwa bei poa.
“Tumepanga
kutengeneza simu zenye kiwango cha juu
zaidi zinazokuwezesha kufanya mambo mengi zaidi siku nzima. Tumefanya hivyo
katika Y6 Pro ambayo ilizinduliwa mwezi Mei na pia katika matoleo mbalimbali ya
simu za Y series yaliyozinduliwa mwezi huu. Matoleo ya Y ni mahususi kwa ajili
ya watumiaji wa simu za kisasa”.
Akielezea
juhudi zinazofanywa na Huawei, Bw. Edmund Gulay mfanyabiashara aliyetembelea
maonyesho ya Saba Saba alikuwa na furaha kuona Huawei wamekuja na matoleo ya Y
kwa gharama nafuu na simu imara za kisasa za Y3II, Y3Lite, Y3 C and Y6Pro
hususani katika kipindi hiki ambacho kila mtanzania anaharakisha kupata simu
orijino katika nchi yetu ambapo wengi wao ni watu wa kipato cha chini na cha
kati.
Katika
nyakati hizi ambazo watanzania wanauhitaji wa simu bora na zinazodumu, huku
TCRA wakiendela na zoezi la kuzima simu zisizo halisi, na katika hitaji la
kuweza kufikiwa bila ngarama kubwa kulingana na mahitaji ya kila siku ya
kimaisha na shughuri za kibiashara, matoleo ya Y ya Huawei ndio chaguo pekee la
watanzania.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)