Pages

Bayport yachangia milioni mbili kwaajili ya ujenzi wa shule ya sekondari Lindi

Meneja wa Bayport Financial Services, Tawi la Lindi, Lovin Mapunda, mwenye fulana juu ya jukwaa, akitoa msaada wa Sh Milioni mbili katika harambee ya kuchangia ujenzi wa shule ya sekondari Lindi iliyoungua, ambapo harambee hiyo iliongozwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa, wa pili kutoka kushoto mstari wa mbele, akifuatilia jambo wakati Meneja wa Bayport Financial Services, taasisi inayojihusisha na mikopo, tawi la Lindi, Lovin Mapunda, hayupo pichani wakati anatoa jumla ya sh Milioni mbili kwa ajili ya mchango wa taasisi yake kwa shule ya Sekondari Lindi, iliyopata balaa la kuungua kwa baadhi ya majengo yake. Picha na Mpiga Picha Wetu, Lindi.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)