Wahudumu wa sekta mbalimbali za kijamii wilayani Uyui Mkoani Tabora na Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Ilolangulu mkoani humo wameanza kunufaika na mradi wa Millenium Village unaowawezesha kuunganishwa na kujifunza kupitia wa mtandao wa Airtel kwa huduma za Internet na za simu ya bila malipo.
Hayo yamebainishwa na Wahudumu wa sekta za Elimu, Afya, maji na Kilimo baada ya Kampuni ya simu za mkononi Airtel kuwapatia msaada wa laini za simu na kuwaunganisha kwenye huduma za internet na kupiga simu bila malipo yoyote. Mradi wa millium village ulianza toka mwaka 2013 kwa lengo la kuwawezesha watoa huduma waishio vijijini kukusanya takwimu za kila mwezi kwa njia ya mtandao, kupatiana taarifa za utekelezaji wa kazi zao na kuwafikia wanufaika kwa urahisi
Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya Wahudumu wa sekta hizo wamesema wameendelea kunufaika huduma za Airtel chini ya mradi huo na kuzitumia vyema katika utekelezaji wa kazi zao
“mpango huu umeturahisishia kutoa huduma za afya kwa jamii ya mbola hususani kwa wamama wajawazito na watoto kwani tunapowatembelea majumbani mwao tunaweza kuwasaidia kwa kuwasiliana na wenzetu kirahisi na pia kuchukua takwimu zao na kuziweka kwenye application maalumu ijulikanayo kama CommCare Application na taarifa zao zinasomeka kirahisi na kwa wakati katika vituo vyetu vya afya. tunashukuru sana Airtel kutupatia huduma hizi bure kwani mawasiliano ya simu ni muhimu sana na yanachochea kuwa na jamii yenye afya bora kwani toka mwaka 2013 hapa mbola hatujawahi kuwa na kifo cha mama mjamzito na mtoto mchanga alisema Mhudumu mkuu wa afya vijijini katika cluster ya ndola , Charles Masanja”
Naye Kaimu mkuu wa shule ya Ilolangulu, Jumanne Mailani amesema kupitia mtandao wa Airtel na chini ya mradi wa (Airtel Connect to lean) Wanafunzi wanauwezo wa kupata taarifa mbali mbali za kimasomo kutoka ndani na nje ya nchi na hivyo kuongeza uelewa na ufaulu shuleni hapo. Lakini pia wanafunzi wetu wanapata fursa ya kujifunza masomo ya komputa na kuunganishwa na huduma za internet na kupata nyenzo zaidi zinazowaongezea maarifa katika masomo yao.
Kwa upande wake Ayub Kim , Mraditi wa kitengo cha miundo mbinu Milllenium Promise Tanzania alisema “Tunashukuru sana Airtel kwa kushirikiana nasi kupitia program hii ya Milllenium Village ambapo mpaka sasa huduma za Airtel zimekuwa msaada mkubwa katika kuendesha huduma mbalimbali hapa mbola na kuwafikia wakazi zaidi ya 45,000.
Tumeanzisha Saccos yetu ambayo pia inaendeshwa kwa kutumia mtandao wa bure wa internet na simu kutoka Airtel na pia tumepata mavuno mengi sana toka kwa wakulima kwani tunaowatoa huduma ambao wanatoa elimu kwa wakulima ili kuinua kilimo chao. Kwakweli tumepata mafanikio makubwa kwani tunawawezesha watoa huduma katika sekta mbalimbali kama vile , kifedha, kilimo,elimu , maji na afya kunufaika na huduma hizi za mawasiliano za Airtel na kuongeza ufanisi zaidi.
Ayub Kim , Mraditi wa kitengo cha miundo mbinu Milllenium Promise Tanzania, akitoa mafunzo ya komputa kwa baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya Ilolangulu mkoani Tabora, wanafunzi hawa wamewezesha huduma za mawasiliano na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel chini ya mradi wa millennium village.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)