AIRTEL KUWAPIGA MSASA WASIMAMIZI WA VITUO VYA VIJANA KWA AJILI YA KUIBUA VIPAJI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

AIRTEL KUWAPIGA MSASA WASIMAMIZI WA VITUO VYA VIJANA KWA AJILI YA KUIBUA VIPAJI

KATIKA kukuza soka la vijana na kuibua vipaji, Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel wameandaa semina elekezi kwa wasimamizi wa mikoa wa vituo vya kukuzia vijana na kuwataka kutumia nafasi hiyo kuinua na kuleta mwitikio kwa vijana wadogo.

Akizungumza katika ufunguzi wa semina hiyo, Afisa Mahusiano wa Kampuni hiyo, Jane Matinde amesema kuwa huu ni mwaka wa 11 toka kuanza kwa mashindano hayo na wamefarijika kuona vipaji vinaibuliwa na Airtel Rising Star imefanikiwa kwa hatua kubwa sana. "Tumefanikiwa kwa kipindi na tunawaomba vijana kujitokeza kwa wingi kuja kujisajili  na semina hii imejikita katika kusimamia kanuni na sheria za mchezo wa soka".

Amesema mara nyingi katika mashindano ya vijana kumekuwa na vitendo vya udanganyifu hasa kwa upande wa umri wa wachezaji na hivyo kwa mwaka huu tumeamua kufanya semima hii ili kuondokana na tatizo hilo.

Katibu mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Mwesigwa Selestine ameipongeza Kampuni ya mawasiliano ya Airtel kwa kuendelea kuthamini michezo.  Ameyasema hayo katika semina ya viongozi wa soka wa mikoa iliyoandaliwa na kampuni hiyo.

Amesema makampuni mengi yamekuwa yakiwekeza zaidi kwa vijana walioibuliwa tayari tofauti na Airtel ambao wamejikita katika kuibua vipaji vya vijana kwani Tanzania kuna vipaji ambavyo havijaibuliwa lakini kupitia michezo wameweza kuonekana na kudhihirisha vipaji vyao.

Pia wamekuwa wakileta ushindani wa kimichezo na kufanya vijana kuzidi kujituma ili kutimiza ndoto zao katika michezo."Tumezoea kuona makampuni mengi kujikita zaidi katika wachezaji wenye majina makubwa hivyo ni jambo la kupongezwa sana kwa hiki kinachofanywa na Airtel", amesema Mwesingwa

Aidha amewataka viongozi wa michezo kuzingatia maandalizi mazuri ili kuepukana na vitendo visivyofaa katika michezo.
Afisa Mahusiano wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel , Jane Matinde akizungumza wakati wa semina hiyo.
Katibu mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Mwesigwa Selestine akizungumza wakati akitoa pongezi zake kwa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa jitihada zao za kuinua vipaji vya soka kwa vijana nchini.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages