Kwa ufupi Women Charity Group ni kundi la wanawake na mabinti wanaomtumikia Mungu kupitia maombi, kuombea Familia,Taifa na mambo mengine mengi . Pia hufanya kazi za kujitolea katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Hospitali ya Ocean Road ambapo walitoa msaada kwa watu wenye Saratani mwaka 2014, mwaka 2015 walitembelea Mburahati kwa watoto yatima waishio na masista, mwaka huu wameweza kwenda Muhimbili kutoa msaada kwa watoto wenye matatizo ya vichwa kujaa maji na mgongo wazi.
Wanakikundi cha Women Charity Group wakiwa wanaingia katika Hospitali ya Muhimbili pamoja na Baadhi ya vitu vyao walivyokwenda kutoa msaada kwa watoto wenye matatizo ya vichwa kujaa maji na migongo wazi.
Baadhi ya wanakikundi cha Women charity group wakitoa msaada katika wodi ya watoto hao.
Mmoja wa wauguzi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili akitoa Shukurani zake baada ya kupokea msaada huo
Kikundi cha Women Charity wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutoa msaada huo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)