Wafanyakazi wa kiwanda cha Bia Serengeti wakiwa katika picha ya pamoja mapema wiki iliyopita mara baada ya kufanya usafi katika mazingira ya Hospitali ya Temeke |
Meneja wa Usalama na Afya kazin wa SBL Bwana David Mwakalobo akimkabidhi vifaa vya usafi Kaimu mganga mkuu wa hospitali ya Temeke |
Mmoja wa wafanyakazi wa kiwanda cha bia Serengeti (SBL) akichangia damu ambapo zoezi hilo la kuchangia damu liliambatana na shamrashamra za kilele cha wiki ya usalama na afya kazini zilizoanzia kiwandani kwa matembezi ya hisani kuelekea katika hospitali ya Temeke |
Dar es salaam ,3 Juni ,2016 ;Wafanyakazi wa kiwanda cha bia cha Serengeti (SBL) leo wamechangia damu katika hospitali ya Temeke jijini Dar es salaam ikiwa ni moja ya mpango ya kampuni kusaidia sekta ya afya nchini.
Uchangiaji wa damu ni moja ya shughuli za kusaidia jamii zinazoendana sambamba na wiki ya afya na usalama kazini kwa kampuni hii,tukio hili linalofanywa kila mwaka likilenga viwanda vya bia na vinywaji vikali kuongeza ufahamu kwa wafanyakazi kuhusu umuhimu wa kuzingatia usalama sehemu za kazi.
Akiwashukuru wafanyakazi wa SBL kujitokeza kwa wingi kuchangia damu Meneja Uzalishaji wa kiwanda cha Dar es salaam Alice kilembe alisema zoezi hili linaenda sambamba na mipango ya kusaidia jamii na lengo ikiwa ni kusaidia kuboresha afya zao.
“Tunapenda kuwashukuru wafanyakazi wote kujitokeza kuchangia damu Tunaamini msaada huu wa damu utasaidia kuokoa maisha ya wale wanaohitaji na pia kusaidia kuboresha afya za watu wetu “alisema Kilembe
Mapema leo Kiwanda cha Serengeti cha Dar es salaam wameshiriki pia katika usafi wa mazingira kuzunguka katika maeneo ya Temeke jambo ambalo meneja uzalishaji wa kiwanda alisema ni “kuitikia wito wa serikali wa kuhakikisha usafi katika maeneo ya wazi”
Kwa mujibu wa Kilembe SBL haijakumbwa na matatizo katika maeneo ya kazi kwa zaidi ya miaka minne ikiwa ni matokeo ya mafunzo ya mara kwa mara kwa wafanyakazi na tahadhari zinazochukuliwa zinazofanya kampuni kukidhi viwango ya kimataifa vya usalama katika mazingira ya kazi.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)