UN yawapiga msasa wanafunzi wa UDOM kuhusu Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

UN yawapiga msasa wanafunzi wa UDOM kuhusu Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs)

Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akiendesha semina fupi kuhusu Malengo 17 mapya ya Maendeleo Endelevu (SDGs) kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) (hawapo pichani) inayoendelea mjini Dodoma chuoni hapa.

Katika kuhakikisha kila Mtanzania anapata elimu kuhusu Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu (SDGs) ambayo yanatakiwa kumfikia mtu mmoja mmoja, ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini (UN) imetoa mafunzo kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), mafunzo ambayo yataweza kuwajengea uwezo kuhusu mpango huo na jinsi unavyoweza kubadili maisha yao.

Akizungumza na MO blog kuhusu mafunzo hayo, Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Bi. Hoyce Temu alisema kuwa mafunzo hayo kwa wanafunzi wa UDOM ni sehemu wa mafunzo ambayo yanatolewa na ofisi ya UN nchini ili kuwawezesha Watanzania kuufahamu mpango huo ambao una malengo ya kubadili maisha ya kila mwananchi, mpango ambao utamalizika mwaka 2030.

Alisema katika mafunzo hayo wametoa elimu kuhusu Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) kwa wanafunzi zaidi ya 200 na hayo siyo mafunzo ya kwanza kwani wameshatoa mafunzo kama hayo kwa wabunge wa Tanzania lakini pia wameshafanya mafunzo kama hayo jijini Arusha ambapo yalihudhuriwa na vijana zaidi ya 200.
Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, ambaye pia ni mmoja wa wakufunzi wa masuala ya SDGs, Hoyce Temu akifafanua jambo wakati wa semina fupi ilihusisha wanafunzi wa UDOM inayoendelea mjini Dodoma.

“Tunataka kila Mtanzania ajue kuhusu Malengo ya Maendeleo Eendelevu (SDGs) tumeshatoa elimu sehemu nyingine hii siyo ya kwanza na tutaendelea kwenda maeneo mengine kutoa elimu zaidi na katika hilo ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini ipo imejipanga kufanya hivyo,” alisema Bi. Temu.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages