Gari la polisi likimwaga maji ya kuwasha, kuwatawanya mashabiki wa soka walioamriwa kurudi nyumbani baada ya uwanja wa taifa kujaa "pomoni" majira ya saa sita mchana Juni 28, 2016. Yanga ilikua ikicheza na timu ya TP Mazembe ya DCR ambapo mpira ulimalizika kwa Yanga kukubali kichapo cha Goli 1 kwa 0 kwenye michuano ya kombe la Shirikisho la CAF hatua ya robo fainali. (PICHA NA K-VIS MEDIA/KHALFAN SAID)
NA K-VIS MEDIA
UONGOZI wa uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam, umelazimika kufunga mageti yote ya kuingilia uwanjani humo baada ya uwanja huo kujaa "pomoni" ilipofika saa 6 mchana.
Polisi walifanya kazi ya ziada kuwazuia maelfu ya mashabiki wa soka waliojihimu mapema kufika uwanjani, ili kujionea pambano hilo la soka ambalo Yanga ilitangaza kuwa halitakuwa na kiingilio.
Polisi walilazimika kutumia mabomu ya kutoa machozi na maji ya kuwasha ili kuwatawanya mashabiki hao wa soka ambao licha ya kuwaambia uwanja umejaa na warudi nyumbani ili kuona pambano hilo kupitia matangazo ya moja kwa moja ya runinga.
Hata hivyo mushawishi huo ulishindikana na hapo ndipo polisi walipoamua kufyatua mabomu na kurusha maji ya kuwasha.
Polisi walipata upinzani kidogo baada ya baadhi ya mashabiki kuanza kurusha mawe hata hivyo sio kwa muda mrefu kwani polisi waliongeza jitihada za kuwadhibiti na baada ya masaa mawili jitihada hizo zilizaa matunda
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)