Steve Nyerere Awapongeza Harmonize na Iyobo Kwa Kuwatuliza Wolper na Aunty Ezekiel - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Steve Nyerere Awapongeza Harmonize na Iyobo Kwa Kuwatuliza Wolper na Aunty Ezekiel



Kiongozi wa zamani wa Bongo Movie Unit,  Steve Nyerere amempongeza msanii wa muziki, Harmonize pamoja na dancer wa Diamond, Mosei Iyobo kwa kuwapa utulivu wasanii wenzake wa filamu Aunt Ezekiel na Jacqueline wolper.

Muigizaji huyo ambaye alikuwa MC katika iftar ya GSM iliyofanyika Kigamboni weekend hii na kuhudhuriwa na mastaa mbalimbali, alisema anawashukuru wasanii hao wa muziki kwa uwamuzi wa kuwahifadhi dada zake hao.

“Mimi nashukuru wasanii wa bongofleva kwa kuwahifadhi dada zetu, Aunt yupo poa, na Wolper naona safi,” alisema Steve Nyerere huku akicheka.

Wolper na Harmonize kwa sasa ni wapenzi na kila mmoja anaonyesha anampenda mwenzake, na Aunt Ezekiel na Mose Iyobo ni wapenzi wa muda mrefu na wanaishi kama familia na mtoto wao mmoja aitwae Cookie.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages