Mohammed Ali Afariki dunia - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Mohammed Ali Afariki dunia

Image captionMohamed Ali
Aliyeluwa bondia wa kwanza maarufu mweney asili ya Kiafrika, Mohammed Ali, wa Marekani amefariki leo asubuhi akiwa na umri wa miaka 74.
Kulingana na msemaji wa familia yake, bingwa huyo wa zamani wa uzani wa juu, anayejulikana sana kote duniani kwa sababu ya machachari yake katika ngumi, alifariki katika jiji la Phoenix Arizona, baada ya kulazwa hospitalini Alhamisi.
Alikuwa na matatizo ya kupumua, hali ambayo ilitatanishwa zaidi na maradhi ya Parkinson, ambayo ni hali ya mgonjwa kutetemekatetemeaka.
Taarifa ya familia yake imesema kuwa ibada ya mazishi itafanywa nyumbani kwake Lousville, Kentucky.
Alipozaliwa alipewa jina la Cassius Marcellus Clay.
Image copyrightAFP
Image captionMohamed Ali nyakati za ujana wake
Alipata umaarufu mkubwa aliposhinda medali ya dhahabu katika mashindano ya Olimpiki yaliyofanyiwa Roma mwaka 1960 katika uzani wa uzito wa kadri au light-heavyweight.
Alipewa jina la Utani "The Greatest" na alimtandika makonde Mmarekani mwenzake Sonny Liston mwaka wa 1964 na kushinda taji lake la kwanza la Dunia.
Alikuwa bondia wa kwanza kushinda taji la Heavyweight mara tatu.
Alistaafu mwaka 1981 baada ya kushinda mashindano 56 kati ya 61 aliyoshiriki.
Image copyrightREUTERS
Image captionMohammed Ali
Makundi mbali mbali yamempa sifa kwa uanariadha wake wa kutia fora.
Kundi la waandishi wa habari wa michezo lijulikanalo kama Sports Illustrated lilimtaja kama "Wanariadha wa Karne" ambapo BBC imemtambua kama "Mwanariadha mashuhuri zaidi wa Karne".
Ali alijulikana sana kwa usemi wake wa kutangulia pigano au baada ya pigano.
Aliweza kubashiri matokeo ya masumbwi kwa ustadi wa kuchapana makonde pia.
Image copyrightAP
Image captionMohammed Ali
Mohammed Ali alikuwa mkereketwa wa haki za kibinadamau ambapo atatambuliwa kukabiliana na ubaguzi wa rangi na ushairi wa kuvutia.
Alipoulizwa angalitaka kukumbukwa vipi alisema wakati mmoja: "Kama mtu ambaye hakuwahaini watu wake. Na ikiwa hilo haliwezekani basi nijulikane tu kama mwanandondi mzuri.
Sijali hata usipotaja nilivyokuwa mwenye umbo la kuvutia."Chanzo BBC Swahili

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages