...............................................................................................................................
HASSAN SILAYO
Mfuko wa Pensheni wa LAPF umefanikiwa kusajili wanachama wapya 27, 362 katika mwaka wa fedha wa 2014/2015 tofauti na mwaka wa fedha 2013/2014 ambapo walisajili wanachama 23,228.
Hayo yamesemwa na Meneja wa Elimu na Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF Bw. James Mlowe wakati na mkutano wa waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam.
Bw. Mlowe alisema kuwa mafanikio hayo yanatokana na huduma na mafao bora yenye wigo mpana na kugusa moja kwa moja maisha ya mtanzania ambapo wamepanga kufikia wanachama 180,000 kufikia mwezi June 2016.
Mlowe aliongeza kuwa miongoni mwa sekta zilizoingiza wanachama wapya kwa mwaka 2014/2015 ni Walimu ambapo imetoa wanachama 39,537, Zimamoto na uokoaji wanachama 851, Polisi na Uhamiaji wanachama 415 na Magereza wanachama 205.
Aidha Bw. Mlowe aliongeza kuwa katika kipindi cha mwaka 2014/2015 mfuko huo ulikusanya kiasi cha shilingi bilioni 210.069 ikiwa ni ongezeko la asilimia 31.9, ambapo wamepanga kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 286 billioni kufikia mwezi Juni 2016.
Pia Mfuko huo umesajili waajiri wapya 88 katika kipindi cha mwaka 2014/2015 na unategemea kuendelea kuongezeka siku hadi siku kutokana na mfuko huo kuendelea kuboresha huduma zake.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)