Mtoto Daniel anayetafutwa na wazazi wake.
Mtoto Daniel ambae anatafutwa na wazazi wake amepotea tangia jana huku juhudi kubwa ya kumtafuta inayofanywa na wazazi, ndugu zake zikiwa bado hazijafanikiwa. Maa ya mwisho kijana Daniel alionekana na kijana anayekisiwa kuwa na Umri wa Miaka 7 Eneo la Africana akiwa amechoka huku akimvuta kuelekea njia ya Tegeta.
Tunaomba Watu, Mtu yeyote atakayeweza kumuona basi anaweza kumfikisha Kituo Cha Polisi kilicho karibu nae.Kwa bahati mbaya aliyetuma ujumbe huu katika makundi mbalimbali ya Whatsapp hakuweza kuweka namba zake za simu. Lakini Endapo mtu atamuona basi anaweza kutoa taarifa Polisi au hata Pia Kutoa taarifa kupitia makundi mbalimbali ya Whatsapp ambayo tunaamini pia taarifa itawafikia haraka wazazi au hata ndugu kama ambavyo taarifa ya kupotea kwake ilivyoweza kutufikia sisi na kuamua kutoa msaada wa kutangaza kupitia hapa.
Tunajua ni jinsi gani Maumivu wanayoyapata wazazi wake lakini Tunamuombea kwa Mungu amlinde huko aliko na Malaika wake wamrudishe kijana wetu Daniel Salama Salimini kwenye himaya ya wazazi wake.
Lukaza Blog inatoa pole kwa Wazazi kwa kupotelewa na Mtoto wao Kipenzi lakini tunapenda kuwaambia kuwa Wamwamini Mungu kwa maana Kila hatua wazikabidhizo kwake na kuamini basi Mungu atawatendea.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)