KANISA LA EAGT LUMALA MPYA LA JIJINI MWANZA LINAKUKARIBISHA KATIKA MKUTANO MKUBWA WA OYES 2016. - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

KANISA LA EAGT LUMALA MPYA LA JIJINI MWANZA LINAKUKARIBISHA KATIKA MKUTANO MKUBWA WA OYES 2016.



KANISA LA EAGT LUMALA MPYA LILILOPO SASABASA ILELEMA JIJINI MWANZA CHINI YA MCHUNGAJI DR.DANIEL MOSES KULOLA, LINAWAKARIBISHA WATU WOTE KATIKA MKUTANO MKUBWA WA INJILI UITWAO “OPEN YOUR EYES AND SEE” KWA KIFUPI “OYES CONFERENCE” UKIWA NA MAANA “FUNGUA MACHO NA UONE” AMBAO HUFANYIKA MARA MOJA TU KWA MWAKA.



MKUTANO HUO UTAFANYIKA KATIKA VIWANJA VYA KANISA LA EAGT LUMALA MPYA KUANZIA SIKU YA JUMAPILI TAREHE 12 MWEZI WA 6 HADI TAREHE 19 MWEZI WA 6 MWAKA HUU, KUANZIA SAA 8 KAMILI MCHANA HADI SAA 12 ZA JIONI.



KATIKA MKUTANO HUO, MHUBIRI WA KIMATAIFA KUTOKA OTTAWA NCHINI CANADA ALIEKUFA NA KUFUFUKA BAADA YA SIKU NNE, MAMA DOMITILA NABIBONE, PAMOJA NA MCHUNGAJI JARED MLOGECHA KUTOKA BOSTON MASACHUSSETS NCHINI MAREKANI, WATAKUWEPO.



WAIMBAJI MBALIMBALI AKIWEMO MASANJA MKANDAMIZAJI KUTOKA JIJINI DAR ES SALAAM, CHAMWENYEWE JEMBE KUTOKA MOROGORO, NA KUTOKA MWANZA HAVILLA KWAYA, HOT SPEARS KWAYA, AGNES AKRAMA,THEO DAV, HAPPY SHAMAWELE, JOSEPH RWIZA,  MITAGATO, SARAH GAGALA PAMOJA NA CHACHA WATAHUDUMU KATIKA MKUTANO HUO.



ILI KUFIKA KANISA LA EAGT LUMALA MPYA, PANDA MAGARI YA AIRPORT AU ILEMELA, SHUKA KITUO CHA SABASABA KONA YA KISEKE, TEMBEA HATUA CHACHE HADI SOKO JIPYA LA SABASABA, ULIZA KANISA LA MCHUNGAJI DR.DANIEL MOSES KULOLA UTAELEKEZWA.



USIKOSE KUFUATILIA MAHUBIRI YA MKUTANO HUO KATIKA RUNINGA YAKO PENDWA YA STAR TV KUPITIA KING’AMUZI JABARI LA VING’AMUZI CHA CONTINENTAL PAMOJA NA 96.8 AFYA RADIO.



WALETE WAGONJWA NA WENYE MAHITAJI MBALIMBALI ILI WAFUNGULIWE KWA JINA LA YESU. KWA USHAURI NA MSAADA WA KIROHO, WASILIANA NA MTUMISHI WA MUNGU, MCHUNGAJI DR.DANIEL MOSES KULOLA, KWA NAMBARI ZA SIMU 0767 74 90 40 AU 0784 74 90 40
Bonyeza Hapa Kusikiliza Au Play Hapo Chini.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages