Balozi wa Huawei Brenda Muchunguzi(Kushoto) akimuonyesha mteja wa Huawei Bw. Wilson Tendwa(Kulia) ubora wa simu mpya ya GR5 katika duka la Huawei lililopo J Mall Dar es Salaam.
Balozi wa Huawei Brenda Muchunguzi(Kushoto) akimuonyesha mteja wa Huawei Bw. Wilson Tendwa(Kulia) ubora wa camera ya simu mpya iliyozinduliwa ya GR5 katika duka la Huawei lililopo J Mall Dar es Salaam.
Balozi wa Bw. Didas Masawe (Kulia) akimuonyesha mteja wa Huawei Bw. Christopher Andrea (Kushoto) ubora wa simu mpya iliyozinduliwa ya GR3 katika duka la Huawei lililopo City Mall Dar es Salaam.
Balozi wa Huawei Jamila Feruz (Kulia) akimuonyesha mteja wa Huawei Bw. Jacob Kaiza (Kushoto) ubora wa simu mpya iliyozinduliwa ya GR3 katika duka la Huawei lililopo City Mall Dar es Salaam.
Huawei
yaleta teknolojia ya juu ya utambuzi wa alama za vidole kwa simu Tanzania
Huawei
kukidhi mahitaji ya kizazi kipya na simu zenye gharama nafuu.
Dar
es Salaam, Juni 2016: Baada ya mafanikio katika uzinduzi wa simu inayodumu
na chaji kwa zaidi ya masaa 90 ya Y6 Pro
nchini Tanzania hivi karibuni; Huawei, kinara wa uvumbuzi ulimwenguni
katika mawasiliano na teknolojia, wamezindua simu mbili za bei nafuu, Huawei GR
3 na GR 5 katika soko la Tanzania mwezi huu. Miongoni mwa bidhaa zingine, simu
hizi zinalenga vijana na watu mbalimbali nchini Tanzania ambao wanakuwa na
shughuli nyingi kwa siku.
Vijana ndio waliohamasisha muundo wa simu
ya GR 3 Na GR 5. Simu hizi mbili zimeundwa mahususi kwa ajili yao. Na
haijalishi una umri gani ila kama una ashiki ya ujana basi we ni kijana; Muundo
wa simu hizo mbili unazifanya kuvutia Zaidi hii ni kutokana na kifaa chenye Uwezo
wa kutambua alama za vidole za mtumiaji kwenye GR 5 na kamera ya MP 13 kwenye
GR 3. GR 5 ni simu rahisi kutumia, ikiwa na muundo wakumsaidia mtumiaji awe na
matumizi rahisi.
Akiongea kuhusiana na simu hizo mpya,
Mkurugenzi wa mauzo ya rejareja wa Huawei
Tanzania Bwana Slyvester Manyara alisema Huawei GR 3 na GR 5 zimetengenezwa ili
kuendana na vijana katika shughuli zao za kila siku kuanzia muundo wake mpaka
matumizi. “Huawei inafikiria daima namna
mpya za kuboresha huduma kwa wateja wetu na tunafuraha kuwa tunafanikisha jambo
hili” alisema Bwana Manyara.
Akiongelea mabadiliko ya matumizi ya
simu za mkononi nchini Tanzania Bwana Manyara alisema mwanzoni simu hizi za
kisasa zilitengenezwa kwa ajili ya watu wenye fedha na kazi za kipato kikubwa
ambao wangeweza kumudu bei, kwa ujumla Huawei imejitahidi kuwepo na simu za
smartphone kwa kila daraja la wateja bila kujali kipato chao. Tukiwa na lengo
la kufikia watu wa soko la chini hadi la kati, tumeamua kuzindua GR5 na GR3.
Simu hizi zimetengenezwa kukidhi mahitaji tofauti ya wateja wetu tukiangalia
zaidi kipato chao. GR3 na GR5 ni simu za bei nzuri pia zina vitu mbalimbali vya
kuvutia kwa ajili ya watu walio katika maisha ya kawaida na kazi za kuwafanya
wazunguke au kutembea sana.
“Kwa
sasa kuna ongezeko kubwa la mawasiliano ya kijamii nchini Tanzania kama Twitter,
Whatsapp, Instagram na Facebook. Watanzania wengi wanapenda unafuu, wepesi na
urahisi katika mitandao hii kwa ajili ya mawasiliano yao kila siku. Simu za
Huawei zimeundwa vyema na zina fanya kazi kwa ufasaha na zinapatikana kwa bei
rahisi. Simu mpya za kuvutia za Huawei katika mlolongo wake wa G zinarudisha
thamani ya fedha yako”, alikazia Mkurugenzi wa Mauzo ya Rejareja.
Kwa mujibu wa Meneja wa Huawei nchini
Tanzania, Bwana Huxiangyang Jacko, GR5 ina teknolojia mpya ya Uwezo wa kutambua
alama za vidole ambayo huifanya iwe haraka na yenye usalama zaidi ukilinganisha
na matoleo ya awali.
“Uwezo
mkubwa wa kutambua alama za vidole za mtumiaji wa simu uliopo katika GR5 unaleta uwezo mkubwa ambao unaongeza matumizi mepesi
na uelewa mzuri kwa mahitaji ya mtumiaji. Toleo hili la pili la Uwezo wa
kutambua alama za vidole linapelekea ufanyaji kazi wa haraka Zaidi na mwepesi
kuliko toleo la kwanza uliokuwepo katika simu za awali. Inasaidia pia kwenye
kuangalia na kufuta vitu kwa haraka na kupiga picha au kupokea simu haraka”
, alisema Bwana Jacko.
Ikiwa na vitu mbalimbali na muundo wa
kuvutia simu hizi zina vifaa vilivyoundwa mahususi kwa kumuunganisha kijana wa
Kitanzania na simu sahihi. Kwa mujibu wa Huawei Tanzania, simu hizo mbili zina
4G. Pia zina LTE ili watumiaji waweze pakua vitu kiurahisi Zaidi, kuangalia
filamu na simu ina nafasi ya kuhifadhi vitu GB 16.
GR3 na GR5 zisingekua simu za Huawei
bila kuwa na kamera zenye ubora wa juu. Kamera zinauwezo wa kupiga picha kwenye
mwanga hafifu na kutoa picha za viwango vya juu. Huawei GR3 Na Gr5 inawapa
watumiaji uwezo kuiona dunia kwa uwezo mkubwa zaidi.
Kwa maneno ya Chades Charles Lwamlema,
kijana wa kitanzania anayefanya kazi katika moja ya mashirika ya kiserikali
nchini, amesifia Huawei Tanzania kwa hatua kubwa waliopiga kufikia kizazi cha
sasa kwa simu za kisasa za bei rahisi, simu ambayo imemsaidia katika kazi yake
na maisha yake kwa ujumla.
Ushuhuda wa uwezo mzuri wa Huawei GR3
na GR5 unaendeleza nia ya dhati ya Huawei kuwa na simu zenye ubora mkubwa katika
soko.
Kuhusu Huawei
Huawei
huongoza duniani katika Teknologia ya Mawasiliano. Ikibuni wakati wote kwa
kuzingatia mahitaji ya wateja, wamejikita katika kuongeza uzoefu wa wateja na
kuleta thamani ya juu kwa mashirika ya simu, makampuni na wateja. Vifaa vya
mawasiliano ya simu ya Huawei, bidhaa za Teknologia ya Mawasiliano, na simu za
kisasa hutumika katika nchi 170 ulimwenguni. Huawei ipo nafasi ya 3 katika
usambazaji wa simu (2015) ilikiwa
imesambaza zaidi ya simu milioni 110 ulimwenguni. Huawei Tanzania imedhamiria
kuwa kinara katika bidhaa borana za kisasa ulimwenguni, ikiwa inatoa huduma za
simu internet rahisi zaidi kutumiwa na wateja. Kwa sasa, Huawei Tanzania ipo
nafasi ya 2 ikiwa na hisa za soko la 22% (katika robo ya kwanza ya mwaka 2016)
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)